Tuesday, January 31, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 31

SIKU YA 31 - 31/01/2017
NINAMSHUKURU BWANA, KWA KUSIKIA NA KUJIBU MAOMBI YANGU
MUNGU HUWA ANAJIBU MAOMBI, HAKUNA OMBI LOLOTE AMBALO MUNGU HAKUWAHI KUJIBU

MAANDIKO YAWEKA WAZI…

Mathayo 7:8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
*Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
MUNGU HASIKII TU LAKINI HUSABABISHA NAFASI YA TUKIO ULILOOMBA LIWE HALISI

Zaburi 118:5 Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.
MUNGU ANA NJIA YAKE YA KUHAKIKISHA ANATUPA MAHITAJI YETU HATA KAMA TUMEISHIWA MBINU KABISA…

Warumi 11:33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
EE MUNGU AHSANTE KWA MAOMBI HAYA (TAJA MAMBO ULIYOYAOMBEA)………….. NA KWA KUWA WEWE UNAJIBU NA HATA SASA UMEJIBU… NIMEYAPOKEA YOTE NILIYOOMBA.. NAISHI KATIKA AHADI ZANGU AMBAZO NI ZA KWELI DAIMA… KATIKA JINA LA YESU
Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu 

TUONANE JUMAMOSI HII MLIMANI DULUTI, WALETE WENYE MAHITAJI AU UKIWA NA HITAJI LAKO TUPATIE TUKUOMBEE

AMEN

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Monday, January 30, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 30

SIKU YA 30 - 30/01/2017

NINAMSHUKURU BWANA, NAMPA DHABIHU ZA KUSHUKURU

Zaburi 50:14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
Zaburi 50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.

Zaburi 54:6 Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.

Zaburi 56:12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.

Zaburi 107:22 Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba.

Zaburi 116:17 Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana;

Yona 2:9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.

Amosi 4:5 mkachome sadaka ya shukrani, ya kitu kilichotiwa chachu; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari na kuzihubiri habari zake; kwa maana ndivyo viwapendezavyo ninyi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana MUNGU.

KAMA UMEPITIA MISTARI HIYO, KUNA MAMBO KADHAA YANAAMBATANA NA KUSHUKURU

1… KUONDOA NADHIRI ZAKO KWA BWANA….

2… KUTENGENEZA MIENENDO YAKO….

3… KUYASIMULIA MATENDO YAKE…

4… KULITANGAZA JINA LAKE…

5… KUIMBA…

6… KUTOA SADAKA ZA HIARI…

KWA UFUPI NI TENGENEZA MAMBO YAKO YA NDANI- NYUMA YA PAZIA (Kama una njia ambazo unajua hazimpendezi BWANA, NA KUSHUHUDIA WENGINE MATENDO MAKUU YA MUNGU, WOKOVU WAKE N.K.)
2 Mambo ya Nyakati 33:16 Akaijenga madhabahu ya Bwana, akatoa juu yake dhabihu za sadaka za amani, na za shukrani, akawaamuru Yuda wamtumikie Bwana, Mungu wa Israeli.

SADAKA YA SHUKRANI INAWEZA KUWA YA MANENO/WIMBO (Nehemia 12:46, Yona 2:9, Yeremia 30:19) AU MALI (2 Nyakati 33:16) AU VYOTE (2 Wakorintho 9:11) inategemea msisitizo wa Roho Mtakatifu ndani yako…

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 28

SIKU YA 28 - 28/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

EE BWANA NIKO TAYARI KUONGOZWA NA WEWE = MPANGO WAKO UWE WANGU
Mara nyingi tunakuwa na mipango yetu mizuri sana (ni muhimu sana kupanga na kuwa na malengo) LAKINI Mungu ndiye anayejua kiasi gani mipango yetu imenyooka au kupinda, yanapoteza au tumepatia… Hivi karibuni nimegundua kwamba kila nilipoomba maelekezo kwa njia ya maombi kuna mambo mengi Mungu ameyabatilisha tofauti na nilivyopanga.. LAKINI mabadiliko hayo yamenipa matokeo ambayo sikuyapata kwa KUHENYA/ NO STRESS

Unajua huwa hatuombi ili tumfanye Mungu abadili mawazo yake na kufuata ya kwetu? Tunaomba ili tuweze kujua na kufuata mpango thabiti aliyoweka kwa ajili yetu…

Isaya 55:8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.

NI SAWA KABISA, LAKINI NAPENDA MAWAZO (PLANS) YA MUNGU KWANI YAKO JUU SANA..

Isaya 55:9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.


UHONDO NI PALE TUNAPOPANGA MAWAZO YA KUTUFANIKISHA KUMBE MUNGU NAYE ANA MPANGO HUO HUO…

Kama LENGO ni KUFANIKIWA Mungu naye hayuko mbali na MPANGO wa kutimiza hilo lengo..

Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo [PLANS] ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani [PROSPERITY] wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. [FUTURE]

Pale neno MAWAZO limetumika kama PLANS = MIPANGO…

Haya MAWAZO/MIPANGO Bwana anaweza kutufundisha kabisa

Zaburi 32:8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

NA LENGO LAKE LA KUTUFUNDISHA NI KUTUFAIDISHA………… HALELUYAH……

Isaya 48:17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

MUNGU HATAKI TUPITE NJIA AMBAZO HATUPASWI KUPITA KABISA… SIYO KILA MPANGO NI WA KUFUATA HATA KAMA WAONEKANA MZURI KWA MACHO NA AKILI nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata
EE BWANA, NINAOMBA UNIFUNDISHE MIPANGO YAKO YENYE FAIDA, NIONYESHE MKAKATI ULIONAO JUU YA MAISHA YANGU, MAWAZO/MIPANGO YAKO IWE MPANGO YANGU, NAREJESHA MIPANGO YANGU YA 2017 CHINI MAPITIO YAKO, UYACHUNGUZE NA KUONDOA LOLOTE LENYE KULETA HASARA/KUANGAMIZA, NITAPITA TU NINAPOPASWA, EE BWANA NISAIDI KWANI Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti [Mithali 14:12, Mithali 16:25] NAMI SITAKI KUPITA HUKO, KATIKA JINA LA YESU

UNAWEZA KUOMBA MAOMBI HAYA JUU YA MKE/MUME WAKO, RAFIKI, NDUGU, AU MTU YEYOTE AMBAYE KILA AKIPANGA MAMBO YANAMWENDEA KOMBO KATIKA JINA LA YESU ATAPATA MPENYO KATIKA MAISHA YAKE…

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Friday, January 27, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 27

SIKU YA 27 - 27/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA


EE BWANA, NISAIDIE KUTOKUAMINI KWANGU

Umewahi kumwamini Mungu kukufanyia jambo Fulani, mwanzoni halafu baadaye unaona huwezi tena kushikilia Imani yako?

Umewahi kuamini Mungu kufanyia jambo kubwa lakini baadaye hali inakuwa tofauti na kuamini hata KUTAKA au kuamua kubadili ukiri wa Imani yako?

Umewahi kuamini jambo kubwa lakini siku zinavyozidi kwenda mbele, umeanza kushusha kiwango ulichokuwa unataka? Au hata kuomba.. Aaah! Vyovyote itakavyotokea I don’t care?

WAKATI MWINGINE IMANI YAKO INATIKISWA KWELI KWELI MPAKA UNAHISI INANG’OKA KABISA…

Maandiko yanasema Waebrania 11:13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.

Badala ya kukata tamaa…. AMINI HADI KUFA WALA USIBADILI UKIRI WAKO… Imani haiko juu ya kile unachokiona bali kwa Mungu na Mungu aweza kufanya lolote kwa wakati wowote… kujidhihirisha kwamba yeye ni Mungu… 

Baba yake kijana aliyekuwa anateswa na mapepo alimwambia Yesu Marko 9:24 …. Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.

CHA AJABU YESU ALIMSAIDIA…. …… akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
HATA PETRO ALIPOANZA KUTEMBEA JUU YA MAJI… Akaona mazingira yakamtia hofu na akaanza kupoteza Mathayo 14:29-31 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

WAKATI WOWOTE KWENYE MAISHA UNAPOINGIA KATIKA MASHAKA NA IMANI YAKO HAIWEZI KUSHIKA NETWORK VIZURI…. Mwambie Yesu… niokoe, ninazama nikijiona…
Sijawahi kuona rafiki kama Yesu HATA IMANI ZETU ZINAPOTINDIKIWA HAJAWAHI KUSHINDWA KUTUSAIDIA…

ANGALIA MADHARA YA KUTOKUAMINI……… Mathayo 13:58 Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.

TENA ANASTAAJABU TUSIPOAMINI Marko 6:6 Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao.

TAARIFA SAHIHI NI MUNGU ANAPENDA SANA KUTUSAIDIA KATIKA HALI ZETU IJAPOKUWA ATAKEMEA UPUNGUFU WA IMANI ZETU…

EE BWANA YESU…NISAIDIE KUTOKUAMINI KWANGU KATIKA (……………..Taja hayo mambo)….

IMANI YA YESU IWE IMANI YANGU….. KUMBUKA HATUAMINI KWENYE MATOKEO.. TUNAAMINI KWA MLETA MATOKEO…. MUNGU… NA YEYE ANADUMU WA KUAMINIWA…
NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 26

SIKU YA 26 - 26/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

NAKATAA KUISHI KAMA WA ULIMWENGU HUU, MIMI NI RAIA WA MBINGUNI

Kuna changamoto kubwa sana mtoto wa ufalme wa Mungu anavyoishi na kuamua kuishi mfumo wa maisha yanayofanana na mtoto wa ulimwengu… MATATIZO YAO YANAFANANA, MIFUMO YA MAISHA, AINA YA MALALAMIKO, AINA ZA MAJANGA, N.K… 

TAARIFA: WEWE SI WA ULIMWENGU HUU

Angalia Yesu anachosema kwenye maombi yake akituombea. Yohana 17:9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako

UKIMPOKEA YESU… UMEKABIDHIWA KWA YESU… NA ULIMWENGU HAUKUTAMBUA HATA KAMA UNAISHI HUMO.. Akanongeza kusema… wao wanatakiwa kuongozwa na NENO la Kristo na siyo wa ulimwengu… 

Yohana 17:14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Sasa kama sisi siyo wa huku, Kwa nini tusiende kwetu..? YESU ALIJIBU HILO… Yohana 17:18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. WE ARE HERE FOR A MISSION.. SISI NI MABALOZI WA UFALME WA MUNGU (NYUMBANI KWETU)

TENA YOHANA AKAONGEZA KWENYE BARUA YAKE… 1 Yohana 4:4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. NDIYO MAANA PAULO AKASEMA Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamili KUGEUZWA UPYA NIA KWENYE KUFUATA NAMNA (PATTERNS) ZA DUNIA HII BALI NENO LA MUNGU LIWE ….. taa ya miguu ZETU, Na mwanga wa njia ZETU. Zaburi 119:105

ANGALIA JINSI WANA ISRAELI WALIVYOTOFAUTISHWA….NA ULIMWENGU MWINGINE… HII NI PICHA HALISI YA MAISHA YETU…

Mwanzo 47:27 Israeli akakaa katika nchi ya Misri, katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali humo, wakaongezeka na kuzidi sana

Walipokaa Gosheni waliongezeka na kuzidi sana JUST IMAGINE

NA PINDI MAJANGA YALIPOACHILIWA KATIKA NCHI… WALITOFAUTISHWA… Kutoka 8:22 Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi Bwana kati ya dunia KWA HIYO MUNGU ANAJIONYESHA KUWA NI MUNGU KWA KUWATENGA NA MAJANGA YA MISRI…

HATA MVUA YA MAWE ILIVYOPIGA PIA…IMEANDIKWA… Kutoka 9:26 Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe

JE, WAJUA Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Mathayo 5:14 NA NDIYO MAANA ULIMWENGU UNAWEZA KUWACHUKIA KAMA WAMISRI WALIVYOFANYA KWA WAISRAELI Yohana 15:18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.

NDIYO MAANA KUNA MAJIPU YA MISRI ILA HAKUNA MAJIPU YA ISRAEL Kumbukumbu la Torati 28:27 

WAKATI FULANI TUNAJISAHAU AU HATUKUJUA YA KUWA TUNAWEZA KUJITENGA NA MAJANGA YANAYOIKUMBA DUNIA KWA KUAMUA KUFUATA MFUMO WA NENO LA MUNGU KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU….

EE BWANA KWA ROHO WAKO MTAKATIFU, NISAIDIE KUISHI KAMA mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, ILI kuzitangaza fadhili zako wewe uliyeniita nitoke gizani nikaingia katika nuru yako ya ajabu, nisiishi kwa kufuatisha namna ya dunia, malalamiko yao, shida zao, changamoto zao. Bali niwe chachu ya kuwasaidia, kuwapa mwanga, niwe jibu la matatizo yao, magonjwa yao, tabu zao, n.k.. niishi kifalme (wa mbinguni) nikitangaza HAKI YAKE, AMANI YAKE, NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU

WE ARE NOT AFFECTED, WE AFFECT. WE ARE AMBASSADORS OF HEAVEN ON EARTH

NB: KAMA HUJAOKOKA MALIZANA NA HIYO BIASHARA.. *MPE YESU MAISHA YAKO KWANZA

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Wednesday, January 25, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 25

SIKU YA 25 - 25/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

BWANA, NISAIDIE KUFANYA MAMBO SAHIHI KWA WAKATI SAHIHI
Umewahi kusikia mtu anaanza biashara ya kuuza sweta wakati wa joto akapata wateja wa kutosha au mtu aliyeuza maua ya Krismasi wakati wa Valentine day? Au Hata kama unataka kusogea na kusonga mbele kwa kasi kiasi gani, hauwezi kupambana kinyume na majira na nyakati ambazo Mungu katika maisha yetu.. Shida siyo nyakati.. ni kutambua wakati uliopo au unaoingia na kusudi la majira au nyakati Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Hii ni kwa sababu huwezi kufanya kitu chochote kikawa kizuri wakati wowote..

Mhubiri 3:11a Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake Sio kwa kutenda tu hata maneno yetu yanafaa SI KILA WAKATI ila kila neno na wakati wake..

Mithali 15:23 Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini! CHANGAMOTO ni pale ambapo hujui majira uliyopo na yakupasayo kufanya ili upate matokeo yatakayoleta SHALOM (Amani, afya, mafanikio, ushindi, n.k) Madahara yake ni kama yale Bwana wetu anayasema juu ya mji huu

Luka 19:44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.

KUTOTAMBUA MAJIRA YA KUJILIWA.. Kwa ufupi, huwezi kufanya maandalizi ya kupokea kitu ambacho hujui kama kinakuja au la…

Luka 19:42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
Mhubiri akaonyesha madhara ya kuwa na uwezo, hekima, maarifa, uhodari, ufahamu bila kujua namna ya kuunganisha FURSA NA WAKATI….

Mhubiri 9:11 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

WAKATI NA BAHATI (FURSA/OPPORTUNITIES) HAZIBAGUI… LAKINI JE, NANI AONAYE JAMBO SAHIHI NA ALIFANYE KWA MUDA SAHIHI?

Danieli 2:21 Yeye (MUNGU) hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa

KWA WAISRAELI ILIBIDI MUNGU AWAWEKEE KABISA KABILA LENYE UWEZO USIO WA KAWAIDA WENYE AKILI za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende

1 Mambo ya Nyakati 12:32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

EE BWANA, NAOMBA UWEZO WA KUTAMBUA MAJIRA NILIYOPO, WAKATI WANGU, NA FURSA SAHIHI ZA WAKATI HUU, NA KUJUA KIPI CHA KUFANYA NA KIPI CHA KUACHA KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU NA HEKIMA YA MUNGU. NIPE AKILI ZA KUJUA NYAKATI, KUYAJUA YANIPASAYO MIMI NA WATU WANGU TUYATENDE ILI NISICHUKULIWE MATEKA KWA UPOTEVU WOWOTE WA KUTOJUA YANIPASAYO

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Tuesday, January 24, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 24

SIKU YA 24 - 24/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

BWANA, NISAIDIE KUONA NA KUTUMIA NILIVYONAVYO

Changamoto na malalamiko ya watu wengi leo ni kudharau vitu walivyonavyo tayari. Watu wengi wanahisi wanakwama kwa sababu hawana baadhi ya vitu.. utasikia mtu akisema sina elimu ya kutosha, sina mtu wa kuniunganishia dili, sina rangi nzuri, sina alama za kuniwezesha, sina mama wa kunishauri, sina mtaji wa kuanza nayo…. NA MUNGU ANAWATAZAMA KWA MSHANGAO AKISEMA NANI ALIYEMWABIA HUYU KAMA VILIVYOKO NJE NDIYO VINAMKWAMISHA?

SINA MKATE, ILA KONZI YA UNGA KATIKA PIPA, NA MAFUTA KIDOGO KATIKA CHUPA

1 Wafalme 17:12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.

HUYU MJANE ALIONA HAPA ALICHONACHO HAKIWEZI KUMSAIDIA NA MARA NYINGI HATUTEGEMEI KUZALISHA TULIVYONAVYO BALI KUZITUMIA NA KUFIA MBELE…

SINA KITU NYUMBANI, ILA CHUPA YA MAFUTA

2 Wafalme 4:2 Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.

ALIDHARAU KWANZA CHUPA YA MAFUTA AMBAYO INGETUMIKA KULIPA MADENI YAKE… KUMBUKA HATA HAKUONA UMUHIMU WA WALE WATOTO WAKE… 2 Wafalme 4:1 ….. akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. LAKINI HUYO ANAYEMDAI ALIONA FURSA YA KUWATUMIA HAO WATOTO WA MJANE….

ALIPOTUMIA USHAURI WA ELIYA 2 Wafalme 4:7 Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.

ALILIPA DENI AKABAKI NA CHENJI……..

MAGWANDA YA SAULI (na silaha za vita) NA KOMBEO LA DAUDI

1 Samweli 17:49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.

MWANZONI ALIJARIBISHA ASICHOKUWA NACHO….. 1 Samweli 17:38-39

Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii. Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua. USIFICHE KIPAWA ULICHONACHO KWA SABABU YA UNG’AVU KILE WALICHONACHO WENZAKO.. 

FIMBO YA MUSA

Kutoka 4:2 Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. WAKATI UNAULIZA NANI ATANIPA KITU CHA KUNISAIDIA MUNGU ANAKUANGALIA NA HIYO FIMBO UNAYOIDHARAU…NDIYO YENYE MUUJIZA WAKO… SIYO KUCHUNGIA MBUZI TU… 

EE BWANA FUNGUA MACHO YANGU, NITAZAME NDANI YANGU, VITU ULIVYOWEKA NDANI YANGU NA KARIBU YANGU IKIWA NI PAMOJA NA MIKONONI MWANGU… NISAMEHE KWA KUVIDHARAU VINGINE NA KUTOTUMIA IPASAVYO.. NIPE NAMNA YA KUTUMIA…USHAURI WA KIUNGU KAMA ULIVYOMPA DAUDI NA KOMBEO LAKE, MAMA MJANE NA CHUPA YA MAFUTA, MJANE NA KONZI YA UNGA NA MAFUTA + WATOTO, FIMBO YA MUSA… NISAIDIE NIFUKUE NILIVYOFUKIA, NIVIPENDE NILIVYODHARAU, NISIMAMIE NILIZOTAWANYA…. KATIKA JINA LA YESU KRISTO

Mithali 17:8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa.

KIPAWA NILICHOPEWA NINAWEZA KUNIPA KILE AMBACHO NIMEKUWA NIKITESEKEA KWA MUDA MREFU

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Monday, January 23, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 23

SIKU YA 23 - 23/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUSHINDA HABARI MBAYA JUU YA HATIMA YAKO

Mara zote unapokuwa kwenye safari ya maono yako… unaweza kukutana na habari za kuvunja moyo kabisa… WENGI WAMEWAHI KUKWAMA HAPA Ndiyo maana nataka tuombe pamoja… Wakati mwingine habari hizo zinaletwa kwa ubaya na siyo kwamba zina uwezo wa kutukwamisha ila jinsi tunavyopokea ndiyo tatizo… Stamina ya kuchukulia poa habari hizo na kuendelea mbele tena wengine huamua kusita na kuacha kabisa kusonga mbele… 

Angalia watu hawa..

1) JOSHUA NA KALEBU VS. WALE KUMI WENGINE

WATU 12 WALIPEWA KAZI YA UTAFITI/UPELELEZI JUU YA NCHI AMBAYO WANA ISRAELI WALITAKIWA KWENDA… 

RIPOTI YA KWANZA Hesabu 13:26-30 Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi.

Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.

Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.

Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.

Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

Hesabu 13:31-33 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

RIPOTI YA PILI

Hesabu 13:30 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

Hesabu 14:6-9 Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, MAANA WAO NI CHAKULA KWETU; UVULI ULIOKUWA JUU YAO UMEONDOLEWA, NAYE BWANA YU PAMOJA NASI; MSIWAOGOPE.

NA WATU WENGI SANA WALIIAMINI ILE HABARI MBAYA ISIYOTIA MOYO…

Hesabu 14:2-4 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri.

Na Mungu naye aliwakasirikia kwa sababa waliamini habari mbaya kuliko ahadi yake…. 

2) NEHEMIA MBELE YA SANBALATI NA TOBIA

NEHEMIA ALIPOANZA PROJECT YA UJENZI WA UKUTA WA YERUSALEMU, HALI HAIKUWA SHWARI… LILIINUKA ZENGWE MOJA MATATA KUTOKA KWA SANBALATI NA TOBIA.. HATUA MOJA BAADA YA NYINGINE… Nehemia 2:19 Lakini waliposikia Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Mtaasi ninyi juu ya mfalme? 

SANBALATI AKAANZA Nehemia 4:1-2 Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.

Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?

TOBIA AKAENDELEZA Nehemia 4:3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe

PAMOJA NA HAYA YOTE… Nehemia 6:15-16 Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu.

3) PAULO NA WAKATISHA TAMAA

Matendo ya Mitume 21:11-12 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.

Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.

CHANGAMOTO INAYOONEKANA HAPA SIYO UJUMBE KUTOKA KWA NABII LAKINI USHAWISHI WAO WA KUMSIHI AISENDE YERUSALEMU…

PAULO AKASEMA… Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu. Matendo ya Mitume 21:13.. KWA HABARI YA PAULO YESU ALISEMA Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. Matendo ya Mitume 9:16 

LAKINI PAULO ALISHINDA…NA KWENDA NA PAMOJA NA MATESO ALIYOPITIA ALIFANYA KAZI KUBWA SANA KAMA ALIVYOTAMKIWA NA BWANA KUPITIA ANANIA… Matendo ya Mitume 9:15 Lakini Bwana akamwambia (ANANIA), Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.

MWAKA 2017, MUNGU AKUPE UWEZO WA KUSHINDA KILA ZENGWE LITAKALOINUKA KATIKA JINA LA YESU… USHINDE HABARI MBAYA KAMA YOSHUA NA KALEBU. USHINDE WAKATISHA TAMAA KAMA PAULO, USHINDE WANAODHARAU PROJECT/MAONO YAKO KAMA NEHEMIA… UNABII WA AGABO USIKUZUIE., HABARI ZENYE HITILAFU ZISIKUVUNJE MOYO..ENDELEA KUMWAMINI MUNGU… DHARAU ZA WENYE UCHUNGU ZISIKUONDOE KWENYE MSTARI…. U MSHINDI KATIK JINA LA YESU

UKISHAJUA UNAPOTAKIWA KWENDA, UKISHAJUA NJIA YAKO….UWE MTU USIYEZUILIKA… BE UNSTOPPABLE

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 22

SIKU YA 22 - 22/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUSHINDWA AU KUACHA KUOMBA/ OVERCOMING PRAYERLESSNESS


Kuna sababu nyingine za watu kuacha kuomba… lakini napenda uangalie kidogo sababu chache kwa nini tunatakiwa kuomba….

KUNA MAMBO MABAYA YANAWEZA KUTOKEA TUSIPOOMBA, KUNA MAJIRA YATATUPA SHIDA, KUNA MAJARIBU TUNAWEZA KUINGIA…

Mathayo 24:20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Luka 22:40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.

YESU ALIKUWA NA KAWAIDA YA KUOMBA AKIMALIZA HUDUMA YAKE… NA NDIVYO ILIVYO KWETU KABISA…

Marko 6:46 Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.

1 Wathesalonike 5:17 ombeni bila kukoma; 1 Samweli 1:12 Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za Bwana, Eli akamwangalia kinywa chake.

MAOMBI SIYO TUKIO LA BAADHI YA SIKU BALI TUNADUMU KATIKA MAOMBI…

Wakolosai 4:2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;

HATA KAMA MUNGU ANAJUA MAHITAJI YETU - ANATAKA TUJIZOEZE KUOMBA KWAKE… UHUSIANO NI MUHIMU… ANAPENDA… TUSEMEZANE NAYE.. Ufunuo wa Yohana 5:8 ……….. kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. 2 Mambo ya Nyakati 1:7 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe.

MAOMBI YANA-ENERGIZE MALAIKA WANAOYUHUDUMIA HASA TUNAPOOMBA MUDA MREFU…

Danieli 9:21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Kutoka 17:11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.

MAOMBI YA ANA NA MZEE SIMEONI YALIACHILIA MALAIKA KIPINDI CHA KUZALIWA YESU…
 Luka 2:34 Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Luka 2:26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

Luka 2:36-38 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.

Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.

KUNA VITU HAVITASOGEA BILA MAOMBI

Marko 9:29 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.

WAKATI MWINGINE MUNGU HUTUPA MAONO TUKIWA KWENYE MAOMBI… FIKIRIA KAMA PETRO ASINGEKUWA NA TABIA YA KUOMBA..

Matendo ya Mitume 10:9-12 Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana; akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi; ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.

MUNGU ANATAKA KUSIKIA HAJA ZETU KABLA YA KUANZA KUWAAMBIA WATU WENGINE… YEYE NI BABA YETU… ANA NJIA BORA KABISA YA KUTUFANIKISHA...

Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

JE, NI NINI KINACHOKUPINGA USIOMBE??

Maombolezo 3:8 Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu.

Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

KUOMBA VIBAYA (KUTOKUJUA) SIYO DHAMBI HUO UDHAIFU ROHO MTAKATIFU ATAKUSAIDIA… ILA USIACHE KUOMBA…


JIFUNZE KUONGEA NA MUNGU MAMBO MBALIMBALI UTAONA FAIDA YAKE…. ACHA KUYABEBA PEKE YAKO… LIWE ZURI, RAHISI, GUMU, JEPESI, MFADHAIKO, MAUMIVU N.K.. 1 Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu ZOTE, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu…… fadhaa zenu ZOTE NA SIYO baadhi……

BABA NAKUOMBA KWA ROHO MTAKATIFU WAKO, NIRUDISHIE TENA KIU YA KUOMBA, KIU YA KUWA NA USHIRIKA NA WEWE, NINAPINGA KATIKA JINA LA YESU KILA KINACHONIPINGA NISIOMBE, NINAONDOA KWENYE MAISHA YANGU KITU CHOCHOTE KINACHONIONDOA UJASIRI WA KUKISOGELEA KITI CHA REHEMA

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 SITAACHA KUOMBA KATIKA JINA LA YESU

NB: JIFUNZE ZAIDI JUU YA MAOMBI NA TAMANI KUWA NA UHUSIANO BINAFSI NA HUYU MUNGU ANAYEKUPENDA SANA…

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 21

SIKU YA 21 - 21/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

2017 NAKIRI NA KUMTAMBUA MUNGU KWENYE MAFANIKIO YANGU

RECOGNITION OF GOD’S PURELY SUPPORT IN OUR SUCCESS

Kati ya jambo gumu litakaloipata kizazi chetu katika nyakati hizi ni watu kuhisi wamejiwezesha kufanikiwa kwa sababu ya kufundishwa sana juu ya SELF-HELP STRATEGIES pamoja na kujaa kwa SELF-HELP BOOKS ambazo zimejikita kuonyesha kwamba MUNGU SIYO MUHIMU kwenye njia ya mafanikio… Lakini KATIKA KWELI YOTE Mungu ndiye anayefanikisha na Mungu ndiye anaye-reward kazi zetu zote…

Kinachotufanikisha siyo akili zetu siyo uwezo wetu, siyo connections zetu nk. Bali ni Bwana.. Mithali 3:5-6 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

Pamoja na kwamba Daudi alirusha jiwe kwa kombeo lake hakusema yeye ndiye aliyemuua Goliathi ijapokuwa wanawake mjini walisema 1 Samweli 18:7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.

Katika njia zake, Daudi alimkiri Bwana… ANGALIA ALIVYOFANYA 1 Samweli 17:45-47 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.

UNACHOTAKIWA KUJUA NI KWAMBA 1 Samweli 2:7-8 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.

Hata maandiko mengine yanasema Kumbukumbu la Torati 8:12-13 Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;

USIJE UKAWAHI KUJIONA KWAMBA I MADE IT … MY SELF-EFFORTS…. 

Kumbukumbu la Torati 8:17-18 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

WANA WA ISRAEL PAMOJA NA KWAMBA WALIPIGANA KUELEKEA NCHI YA AHADI LAKINI WALIKUWA MAKINI KUWAELEKEZA WATOTO WAO KWAMBA Zekaria 4:6 Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. 

BALI HII NDIYO HADITHI WALIZOWAAMBIA WATOTO WAO… Zaburi 44:1-3 Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale. Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa, Ukawakalisha wao. Wewe uliwatesa watu wa nchi, Ukawaeneza wao. Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi, Wala si mkono wao uliowaokoa; Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.

ANAYETOA MAFANIKIO NI MUNGU SIYO SHETANI? YA AINA YOYOTE? 

KWA NINI BASI WATU WAKIENDA KWA WAGANGA WANAFANIKIWA?

Adui (shetani) huwa anasimama kupinga watu wa Mungu wasipokee kutoka kwa Mungu wala Yeye hatoi chochote.. (soma Yakobo 1:17, 1 Wakorintho 16:9) Kumbuka Daniel na majibu mazuri ya maombi yake.. Danieli 10:13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi 

KWA HIYO ILI SHETANI AACHIE ANAHITAJI MAMBO MAWILI

1.KUPIGWA ASOGEE NJIANI (Angalia Daniel aliendelea kupigana na malaika nao wakawa kazini) 
2.KUABUDIWA/KUSUJUDIWA- Ndiyo maana alimwambia Yesu.. amsujudu ili apewe vyote bila fight yoyote.. Luka 4:7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

OPTION YA PILI NI RAHISI LAKINI INA MADHARA MAKUBWA HUWA ZINAWATOKEA PUANI.. 

Ya kwanza ni option sahihi sana…. Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

MUNGU NDIYE KILA KITU… SIYO SHETANI, SIYO NGUVU ZETU, SIYO AKILI ZETU….
NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 SITAISHI KWA KUTEGEMEA AKILI ZANGU, WALA NGUVU ZANGU, NITAMTUMAINI BWANA NAYE ATANITENGENEZEA NJIA, NA KATIKA NJIA ZANGU ZOTE NITAMKIRI YEYE… TUTAWAAMBIA WATOTO WETU, WEWE NDIYE ULIYETUTAJIRISHA, WEWE NDIYE ULIYETUPA VYOTE KATIKA JINA LA YESU

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Friday, January 20, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 20

SIKU YA 20 - 20/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUYAKABILI MAMBO YA SIRI/ATTACKING BEHIND THE SCENE

UNITAKASE NA MAMBO YA SIRI.

Changamoto ya watu wengi ni kuishi vizuri nyuma ya pazia wakati hakuna mtu anayemuona, je umewahi kumuona mtu kabla hajatupa uchafu barabarani anaangalia kwanza ni nani anamuona? KUNA TATIZO mahali…

Hata kama hakuna mtu anayekuona uwe na uhakika Mungu anakuona…. UKIWEZA KUSHINDA UBAYA NYUMA YA PAZIA Ni rahisi kushinda mbele ya kadamnasi…. Ukiingia leo makanisani watu wamebandika BIG G au Bubblish kwenye viti kwa siri bila mtu yeyote kuwaona… HUU NI UGONJWA…. CHARACTER PROBLEM.. Kufanya jambo baya kwa sababu hakuna anayekuona ni hatari sana…

Changamoto ni kwamba MUNGU Huvumbua mambo ya siri tokea gizani, Na hicho kilicho giza tupu huleta mwangani Ayubu 12:22

UKIONA YAMEANDIKWA UJUE YALIVUJA….

2 Wafalme 17:9 Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.

LAKINI PIA MUNGU HUZILETA HUKUMUNI SIRI ZA WANADAMU…


Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

SIYO MATENDO TU HATA MANENO YALIYOSEMWA SIRINI…

Mhubiri 12:14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Lakini Luka 12:3 Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.

NA NDIO MAANA DAUDI AKAONA ASHUGHULIKIE MAMBO YA SIRI…..

Zaburi 19:12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.

NI VYEMA KUMHESHIMU MUNGU NA KUTENDA WEMA SIRINI NA MWANGANI, USIKU NA MCHANA…KATIKA HALI ZOTE…

MAMBO YAKO YA SIRI YAKIWEKWA WAZI UTAKUWA WA KWANZA KUANGALIA?? KAMA SIVYO… MUOMBE MUNGU AKUTAKASE NA MAMBO YA SIRI SASA NA HATA MILELE….

IKIWA UNATAKA KUFIKA MBALI KWENYE HATIMA YAKO… CHANGAMKIA HILI DILI… Ee BWANA Unitakase na mambo ya siri

ATTACKING YOUR BEHIND THE SCENE WHERE NOBODY SEES…

TUOMBE

Ee BWANA Unitakase na mambo ya siri. Uniepushe na ukaidi ninaujua ambao watu hawajui.. nisikutende dhambi eti kwa sababu hakuna anayeniona. Nisipite njia ya mataifa eti kwa kuwa wenzangu hawapo karibu. Ninaomba niwe mtu wa adili maana Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. (Zaburi 112:4). Mimi ni nuru ya ulimwengu Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza (Yohana 1:5). KILA JAMBO NITAKALOLIFANYA NYUMA YA PAZIA LITAENDANA SAWA SAWA NA MAAGIZO NA UKWELI WA NENO LA MUNGU… Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. (Zaburi 19:14)

NIMEJIEPUSHA NA MAMBO YA SIRI YASIYOLETA UTUKUFU KATIKA JINA LA YESU………..

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 NITATEMBEA NURUNI

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Thursday, January 19, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 19

SIKU YA 19 - 19/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

2017 KOMBOA WAKATI NA KUPINGA WANAOKULA MUDA WAKO

NZIGE, NA PARARE, NA MADUMADU, NA TUNUTU, JESHI KUBWA LILILOKULA MUDA WAKO… mwaka 2016 

LAKINI NAJUA UNAWEZA KUKOMBOA… Waefeso 5:16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

NA BWANA ANAWEZA KUKURUDISHIA Yoeli 2:25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

HILI SIYO SUALA LA UMRI ULIOPOTEA BALI NI MATOKEO YA KAZI ILIYOFANYIKA AMBAYO HAIONEKANI….. Mithali 14:23 Katika kila kazi mna faida; I WAPI FAIDA YA KAZI ZAKO??...

Yoeli 1:2-4 Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu? Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine. Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.

UKISOMA MISTARI YA CHINI UTAGUNDUA KUNA VITU VINGI VIMEHARIBIWA Yoeli 1:7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe. ANGALIA TENA Yoeli 1:17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka. ALIPOFIKA MLANGO WA PILI BAADA YA KUMLILIA BWANA Yoeli 1:19 Ee Bwana, nakulilia wewe; Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani, Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.

HAYA NDIYO MAJIBU YAKE…. Yoeli 2:25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

JE, WATARUDISHIWA 2015 AU 2014? HAPANA… NI NGUVU KAZI ILIYOPOTEA
REDEMPTION/RECLAMATION/RESTORATION…

Kwa mfano: Kama ulitakiwa leo….uwe na nyumba na bado huna… na kujenga kikawaida hutumia miezi 6 REDEMPTION hukufanya urudishie kwa speed NYUMBA na vitu ambavyo unatakiwa kuwa nazo leo….ambavyo ADUI ALIZIHARIBU AU KUZIBANIA…

MFANO MWINGINE.. Kama leo ungezaa mtoto mmoja mmoja ulitakiwa kuwa na watoto watatu… REDEMPTION hukupatia MAPACHA WATATU (TRIPLETS) 

Hapa wale ulioanza nao halafu ulipopotea wakakuacha huwa wanajiuliza, kha mbona juzi tu ndo kaanza? 

HAPA SIO KURUDISHIWA SIKU BALI PRODUCTIVITY (MAZAO) YA SIKU ZAKO ZILIZOPOTEA.. 

UKIMUOMBA MUNGU AKOMBOE VITU VYAKO, HIVYO NDIVYO ZITAKAVYOFANYIKA IN JESUS NAME

*NAPINGANA NA KILA JAMBO LINALOWEZA KULA UWEZO WANGU WA KUZALISHA KATIKA JINA LA YESU, NAKOMBOA VYOTE NILIVYOPOTEZA KATIKA JINA LA YESU, NACHUKUA SPEED SAWA SAWA NA NILIVYOPOTEZA KATIKA JINA LA YESU… KILA ZAO LANGU LA HAKI LINANIRUDIA… SITAPOTEZA TENA KATIKA JINA LA YESU*

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 KOMBOA WAKATI NA KUPINGA WANAOKULA MUDA WAKO


SASA OMBA KWA MANENO YAKO

KAMA UNA TATIZO KUMALIZA SIKU HALAFU UNASHANGAA HAKUNA IMPACT YOYOTE YAANI KAMA VILE ULIRUKA SIKU HIYO…OMBA, KEMEA, PANGA MUDA WAKO VIZURI, ANGALIA MUDA WAKO UNAVYOTUMIKA ILI USIPOTEZE TENA, ACHANA NA MAMBO YASIYO NA MBELE WALA NYUMA

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Wednesday, January 18, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 18

SIKU YA 18 - 18/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KULINDWA DHIDI YA MAGONJWA NA UDHAIFU WA KILA NAMNA

Kati ya mambo ambayo Yesu aliyabeba msalabani ni magonjwa na udhaifu wa kila namna, iliyokuwa imestahili kuwa yetu.

Isaya 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu, Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona

Mathayo 8:17 .....Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

Mathayo 4:23......na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna.

Magonjwa ya adui yasiwe juu yako ...

Yohana 10:10 ..Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; Mimi (Yesu) nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele

KILA UGONJWA NA UDHAIFU ULIO KWENYE MWILI WAKO SIO WA KWAKO NI WA ADUI, KEMEA KWA JINA LA YESU

OMBA..

YESU ALIKUJA ILI NIWE NA UZIMA TELE, NINAO UZIMA KATIKA JINA LA YESU, YESU ALIJITWIKA UDHAIFU WANGU, KATIKA JINA LA YESU.

MAGONJWA YA MLIPUKO YASINIPATE, KWA MAJINA YAKE. NIKO CHINI YA UVULI WA MWENYENZI MAGONJWA HAYATANIPATA...

Mwaka 2017 sitaangukia katika MAGONJWA ya aina yoyote..

SASA OMBA KWA MANENO YAKO* KAMA UNA udhaifu AU ugonjwa WA AINA Yoyote, OMBA Kemea

Mungu atakujalia utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
We are the Standards! 2017

Tuesday, January 17, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 17

SIKU YA 17 - 17/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KWA NINI HOFU SIYO KIKWAZO KWAKO

Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

UKIONA UNA ROHO YA HOFU UJUE IMETOKA KWA ADUI KWANI MUNGU HAJAKUPA HIYO ROHO KWA HIYO LAZIMA UPINGANE NAYO

MUNGU HUTUPA roho ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi WALA HATUNA roho wa utumwa iletayo hofu; bali tulipokea (kwa Mungu) roho ya kufanywa wana….. WANA WAKO HURU… 

SABABU KWA NINI HUPASWI KUOGOPA

KUNA SABABU NYINGI ZA WATU KUTAKIWA KUOGOPA...

1 Samweli 22:23 Kaa wewe pamoja nami, usiogope; kwa maana yeye atafutaye roho yangu, ndiye atafutaye na roho yako; nawe utakaa kwangu salama.

2 Wafalme 6:16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.

1. BWANA NDIYE AKUFANIKISHAYE…

Zaburi 49:16 Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.

HAUKO PEKE YAKO BWANA YUKO KAZINI NA WEWE…

Isaya 41:10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

1 Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

YESU ALISEMA Mathayo 28:20 …… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. YAANI JANA, LEO NA KUENDELEA

Zaburi 4:8 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

2. MUNGU ANAWEZA KUKUEPUSHA NA AIBU

Isaya 54:4 Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena

3. KUMTUMAINI BWANA HUONDOSHA MBALI HABARI MBAYA…..NA HATA IKIJA HAUTATIKISIKA WALA KUOGOPA

Zaburi 112:7 Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.

Zaburi 23:4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

4. MALAIKA WAKO KAZINI KUHAKIKISHA USALAMA WAKO WALA HATUJILINDI...

Zaburi 34:7 Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Zaburi 91:5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

5. BWANA NDIYE TEGEMEO LETU SIYO WATU…..HATA KAMA WANAWEZA KUTUSAIDIA BWANA ANAWEZA KUMTUMIA MTU/KITU CHOCHOTE

Waebrania 13:6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

Yeremia 17:7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

Mithali 29:25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye Bwana atakuwa salama. 

Zaburi 125:1-2 Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. 

Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa……….MUNGU YUKO PAMOJA NAMI SIKO PEKE YANGU…. Sitaogopa habari mbaya; Moyo wangu u imara namtumaini Bwana……. walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao… Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami.. Sitaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 NATEMBEA NA KUFANYA MAMBO YANGU KWA UJASIRI..…. MWENYE HAKI NI JASIRI KAMA SIMBA

SASA OMBA KWA MANENO YAKO* KAMA UNA TATIZO LA HOFU AU WOGA WA AINA YOYOTE, OMBA

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
We are the Standards! 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 16

SIKU YA 16 - 16/01/2017
Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KATAA UTASA/KUTOKUZAA KWENYE KILA KITU CHAKO

Kutoka 23:26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.

SIYO KUSUDI LA MUNGU KUSHINDWA KUWA PRODUCTIVE/KUZAA KWANI AHADI YAKE KUTOKUWEPO MWENYE KUHARIBU MIMBA, TASA, WALA KUFA KABLA YA KUMALIZA HESABU ZA SIKU ZAKO…

Ayubu 3:7 Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe

SIKU ZA MTU ZINAWEZA KUFANYWA TASA.. UNAWEZA UKAWA UNAPIGA KAZI KWA BIDII LAKINI UKIFANYA EVALUATION NI KAMA ULIKUWA UNALALA TU NYUMBANI..

Ayubu 15:34 Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.

KATI YA MAMBO YANAYOHARIBU NA KUFANYA WATU KUTOKUZAA NI KUTOMCHA MUNGU NA KUTOA RUSHWA/KUPENDELEA… KWANINI RUSHWA NI MBAYA?

Kumbukumbu la Torati 16:19 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. UWEZO WA KUFIKIRI KIMKAKATI KATIKA HAKI UNAPOTEA…

Zaburi 113:9 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha. LAKINI ASHUKURIWE MUNGU AJUAYE KUBADILISHA MAJIRA..ALIYE TASA AWE MAMA MWENYE FURAHA…

Mwanzo 25:21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba

UNAWEZA KUMWOMBA MUNGU AONDOE UTASA KWAKO NA MKEO (MUMEO) NA PIA KWENYE KILA JAMBO UNAOLIFANYA…

NATAMKA UZIMA JUU YA KILA JAMBO NINALOLIFANYA… HAPATAKUWA NA MWENYE KUHARIBU MIMBA, WALA ALIYE TASA, KATIKA NCHI YANGU; NA HESABU YA SIKU ZANGU BWANA ATAITIMIZA. SIISHI KATIKA RUSHWA NA UPENDELEO WALA KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA… KUTOKUZAA, KUTOKUONGEZEKA HAITATAJWA KATIKA MAISHA YAKO KATIKA JINA LA YESU... KWA SABABU Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 UZAO WAKO UONGEZEKE…. KAMA UNATAKA MTOTO UTAPATA MWAKA HUU

SASA OMBA KWA MANENO YAKO

KAMA UNA TATIZO LA KUTOKUZAA KWA MUDA MREFU OMBA HUKU UMEFUNGA NA USOME, 1 Samweli 1:1-28, Mwanzo 11:30, Zaburi 113:9, Luka 1:36-37

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Saturday, January 14, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 14

SIKU YA 14 - 14/01/2017
Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

NAJITENGA NA UFUKARA NAJIUNGAMANISHA NA UTELE

Kuna watu wanajisikia raha kuwa masikini, lakini pia wanaumia wanaposhindwa kuwasaidia watu wenye uhitaji…. Ni hivi wanafanya kama Yakobo 2:15-16

Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?

Lakini Mhubiri anaongezea pia Mhubiri 9:16 Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi

Kumbukumbu la Torati 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

2 Wakorintho 8:9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

NI MPANGO WA MUNGU KUTAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE…. Kwa sababu ina kazi kwa Mungu 2 Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.

ADUI ANAPENDA UOKOKE LAKINI USIWE NA CHOCHOTE, MUNGU AKAMWAMBIA MUSA Kutoka 3:21 Nami nitawapa watu hao kufadhiliwa mbele ya Wamisri; hata itakuwa, hapo mtakapokwenda zenu hamtakwenda kitupu;

LAKINI FARAO AKA REACT MUSA AKASEMA Kutoka 10:9 Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana sikukuu.

BAADA YA PIGO ………… Kutoka 10:24 Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie Bwana; kondoo zenu na ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi.

KIRI NA UOMBE….. USIMPE ADUI AKUZUIE USIINGIE KATIKA UTELE…
Zaburi 23:1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. KUBALI KUONGOZWA NA BWANA KWANI Zaburi 23:2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

MUNGU amenipa nguvu za kupata utajiri; Nimetajirishwa katika vitu vyote ili niwe na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yangu

Kama Yohana alivyoomba 3 Yohana 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. Zaburi 34:9-10

Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema. WATAKUWA NAVYO TELE

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 UIMARISHWE KWENYE KIPATO CHAKO….


SASA OMBA KWA MANENO YAKO

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Friday, January 13, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 13

SIKU YA 13 - 13/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA
KUSHINDA KUAMBATANA NA WATU WASIO SAHIHI/MAHUSIANO MABOVU

Mithali 7:7 Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,

Sikutegemea kijana huyu awe na akili wakati yuko katikati ya wajinga…. Ndiyo maana ni vyema kumwomba Mungu akupe watu sahihi wa kuambatana nao… .SIMAANISHI WALIOKUZIDI TU BALI WANAOTAKIWA (RIGHT PEOPLE) Mithali 13:20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia

Changamoto ya kwanza ya Balaamu haikuwa uchawi wake bali watu waliombatana nao… ndiyo waliomshawishi awalaani Israeli…

MUNGU ANAMUULIZA BALAAMU Hesabu 22:9 Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?

MUNGU AKUFUNDISHE NA AKUSAIDIE KWA ROHO WAKE MTAKATIFU KUCHAGUA WATU SAHIHI MWAKA 2017

Wakati mwingine macho yanaweza kukudanganya ukaingia kichwa kichwa kumbe kuna hila kwa sababu umeangalia kwa nje tu…

KUNA MTU AKIFANYA “FRIENDSHIP ANALYSIS” UTAGUNDUA TANGU UANZE KUKAA NA BAADHI YA WATU UMEENDELEA AU UMERUDI NYUMA…. UNAONGEZEKA AU UNAPUNGUA… KIU YA KUMTAFUTA MUNGU INAZIDI AU INAPUNGUA… ANGALIA TABIA MPYA ULIYOIPATA… NZURI AU MBAYA???

1 Samweli 18:1 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
MUNGU AKUKUTANISHE NA WATU SAHIHI WA KUAMBATANA NAO KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 UWE NA MAHUSIANO SAHIHI KATIKA JINA LA YESU….

SASA OMBA KWA MANENO YAKO

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 12

SIKU YA 12 - 12/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUSHINDA KUDUMAA/OVERCOMING STAGNATION


Kuna watu wanapita sehemu moja kwa muda mrefu bila kujua kwanini wanashindwa kutoka, au kwa kukosa njia ya kutokea… changamoto kubwa ni pale ambapo wao wenyewe wameanza kuchukia hiyo hali. Hiyo ni dalili nzuri kwamba unatakiwa kwenda mahali pa juu Zaidi… MUNGU ANAWEZA KUKUPA PASSWORDS ZA KUKUTOA HAPO…

Yakobo alikaa kwa Labani akaona amekwama kwa muda mrefu MALAIKA AKAMLETEA FURSA ILIYOMTOA Mwanzo 31:11-12

Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.

Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani.

LABAN ALIBADILI MSHAHARA WA YAKOBO MARA KUMI Mwanzo 31:41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.

Mwanzo 30:43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.

RIPOTI KWA ESAU INASEMA Mwanzo 32:5 nami nina ng'ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako.

BAADA YA KUKWAMA SIKU NYINGI Kumbukumbu la Torati 2:1-2

Ndipo tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia Bwana; tukawa kuizunguka milima ya Seiri siku nyingi.

Bwana akanena, akaniambia,

MUNGU ANAWAPA PASSWORD

Kumbukumbu la Torati 2:3 *Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini.*

YUSUFU ALIKAA GEREZANI MPAKA MUNGU ALIPOMPA PASSWORD YA KUTAFSIRI NDOTO (KUMBUKA HATA ILE YA KWAKE ALIYOIOTA HAKUWEZA KUITAFSIRI BADALA YAKE ALIIPELEKA KWA BABA YAKE) 


MUNGU AKUONGEZE UWEZO 2017 AMBAO HUKUWAHI KUWA NAO…

Mwanzo 41:38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?

Mwanzo 41:42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.

Mwanzo 41:41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.

MUNGU ANAWEZA AKAKUWEKA PANAPO NAFASI…*

Zaburi 31:8 Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.

MUNGU AKUONYESHE FURSA ITAKAYOKUTOA… AKUPE NAFASI ILI UONE NJIA SAHIHI YA KUPITA… KAMA UMEKWAMA SEHEMU MUNGU Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Zaburi 20:2
MWAKA 2017 HAUTAKWAMA KATIKA JINA LA YESU….

SASA OMBA KWA MANENO YAKO


Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Wednesday, January 11, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 11

SIKU YA 11 - 11/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA


Isaya 54:2 Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.

Isaya 26:15 Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

YABESI ALIJUA ANAYEPANUA HOZI (TERRITORY) YA MTU NI BWANA

Habari za Yabesi hazikuandikwa sana lakini maandiko yanaonyesha kuwa Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 1 Mambo ya Nyakati 4:9

1 Mambo ya Nyakati 4:10 [Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishiahozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.]

Mungu atanue nafasi yako katika sekta au nafasi uliyoitiwa, katika territoty uliyopo katika jina la Yesu…


Haijalishi umenenewa nini, umeitwa jina gani, umeaminishwa nini juu yako… Kama Yabesi aliyeitwa na kuungamanishwa na huzuni alichomoka kwa kumuomba Mungu Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishiahozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! IWE KWAKO KWA JINA LA YESU…BWANA ABADILI MAJIRA YAKO.. UPANUKE NA KUIMARIKA PANDE ZOTE..

SASA OMBA KWA MANENO YAKO

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Tuesday, January 10, 2017

MWIMBAJI WA WIKI - JOSHUA SILOMBA

LEO TUKO NA MCHUNGAJI JOSHUA SILOMBA
Mchungaji Joshua Silomba
Rejoice Blog: Labda tuanze kwa kujua majina yako kamili na ikiwa unatumia jina tofauti kwenye kazi zako za muziki?

Joshua Silomba: Naitwa Joshua Silomba wakati mwingine huwa naitwa Pastor Joshua kutokana na huduma yangu ya kichungaji.

Rejoice Blog: Je, umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?

Joshua Silomba: Nimeokoka, ninaabudu kanisa la T.A.G Toangoma na pia ninatumika kama Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo (Mchungaji wa Vijana/Sifa na Kuabudu).

Rejoice Blog: Historia yako kwa kifupi ya kuimba, yaani ulianzaje na wapi ulianzia?

Joshua Silomba: Nakumbuka nilianza kuimba nikiwa mtoto kabisa kule nyumbani Vwawa, Mbozi. Baba yangu alikuwa Mchungaji na familia kwa ujumla ni ya Kikristo hivyo muda mwingi tulikuwa tukiimba nyumbani na kanisani pia hasa kwenye Sunday School. Nilikigundua zaidi kipaji changu cha kuimba nilipoanza kusoma Shule ya Sekondari miaka ya 2000, nilipofika kidato cha pili niliendelea zaidi kugundua uwezo wangu wa kuongoza ibada (kuimbisha), kupiga muziki na pia kutunga nyimbo. Mwaka 2003 nilikabidhiwa rasmi jukumu la kufundisha kwaya ya kanisa la TAG Mji Mkuu nikiwa Morogoro na tangu hapo nimeendelea kumtumikia Mungu katika maeneo yote niliyoyataja hapo juu (Kuongoza ibada, kupiga muziki, kutunga nyimbo zangu binafsi na kwaya na pia kufundisha kwaya na timu za kusifu na kuabudu).

Joshua akiiongoza ibada na sifa kanisani
Rejoice Blog: Katika kuimba kwako, je, umeshatoa albumu yoyote? Majina ya albamu?

Joshua Silomba: Nimewahi kutoa albumu mwaka 2010 iliyoitwa MUNGU WETU HASHINDWI (audio) na kwa sasa nina albumu nyinginei itwayo JAMBO JIPYA (audio) ambayo niliitoa rasmi tarehe 04.12.2016.

Rejoice Blog: Wimbo unaoupenda zaidi kati ya nyimbo zako ni upi?

Joshua Silomba: Kwa kweli napenda nyimbo zangu zote kwa kuwa kila wimbo umebeba ujumbe maalumu na pia sababu maalumu ya kutungwa kwake. Hivyo, kila wimbo una mguso wa kipekee napozisikiliza na kuziimba pia.

Rejoice Blog: Nani anasambaza na kusimamia kazi zako? Na je, anakusaidia vizuri?


Joshua Silomba: Kwa sasa sina msambazaji wala mtu anayesimamia kazi zangu, labda kwa hapo baadaye.

Rejoice Blog: Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na unapenda kufuatilia kazi zake?

Joshua Silomba:    Kwa Tanzania ni wengi wanaonivutia katika muziki wa Injili hususani wanaoimba nyimbo za sifa na ibada. Kwa nje ya nchi kwa sas anapenda sana kumsikiliza na kumfuatilia William McDowell.

Rejoice Blog: Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za Injili?

Joshua Silomba: Mafanikio ninayoyaona kwa sasa ni kupanuliwa zaidi kwa wigo wa kihuduma, watu wengi zaidi wanaendelea kunifahamu na kufuatilia ninachofanya katika huduma yangu. Pia naendelea kuwafahamu na kukutana na wadau mbalimbali wa muziki wa Injili kama vile wazalisha muziki (producers), waongoza video (video directors) na waimbaji ambao wananipa changamoto ya kufanya kazi katika ubora na viwango vya hali ya juu.

Joshua Silomba
Rejoice Blog: Umekutana na changamoto gani katika huduma yako ya uimbaji?

Joshua Silomba: Changamoto ni nyingi ila kwa uchache, nimepata sana changamoto ya kifedha katika kufanikisha malengo yangu ya kihuduma hivyo kufanya kazi zisizona viwango ninavyovitaka, ucheleweshwaji wa kazi studio au kupoteza kabisa (nimewahi kurekodi nyimbo ambazo hadi sasa sijazipata kwa miaka zaidi ya miwili, pia nimewahi kurekodi video ambazo sijawahi kuziona pasipo maelezo yanayojitosheleza). Changamoto nyingine ni kutopata ushirikiano kwa waimbaji wengi waliotangulia kwenye huduma hii ya uimbaji na mwisho, mfumo wa vyombo vya habari wa Tanzania (Redio, TV, nk) hautii sana moyo hasa kwa waimbaji wanaoanza huduma hivyo ziko nyakati ambazo nilikatishwa sana tamaa na mfumo huu.

Rejoice Blog: Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina unayoimba wewe?

Joshua Silomba: Muziki wa Injili Tanzania unazidi kukua na changamoto inazidi kuwa kubwa hasa kwa upande wa ubora na viwango. Lakini pia kwa upande mwingine, muziki wetu umeingiliwa sana na mamluki, hivyo kusababisha waimbaji wengi hata wasio na shida kuonekana ni wababaishaji.

Rejoice Blog: Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili ambao kwa njia moja ama nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii?

Joshua Silomba: Nashauri waimbaji wanaojisahau na kujichanganya na mambo ya kidunia wajitambue na kurejea kwenye misingi ya Neno la Mungu ambalo linatuongoza kupita katika njia za haki na utakatifu. Zaidi wanatakiwa kutubu na kusimama kwenye kweli ili utumishi wao usiwe bure.

Joshua akiiongoza ibada na sifa kanisani
Rejoice Blog: Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unakifanya?

Joshua Silomba: Kama nilivyosema hapo awali, mimi ni Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la TAG Toangoma na nina wajibika zaidi kama Mchungaji wa Vijana na Sifa na Kuabudu (Youth/Worship Pastor). Najishughulisha pia na kilimo, ufugaji na biashara. Pia ni MC kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kikanisa.

Rejoice Blog: Je, kimaisha uko wapi? Ndoa na watoto vipi?

Joshua Silomba: Ninaishi Toangoma, Dar Es Salaam. Nina mke (Bertha) na mtoto mmoja (Doreen).

Rejoice Blog: Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania?

Joshua Silomba: Tupendane, tuwe na umoja na pia tuishi maisha halisi ambayo yatamtukuza Mungu.

Rejoice Blog: Na kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za Injili una ujumbe gani kwao?

Joshua Silomba: Waendelee kututia moyo na kutupa ushirikiano tunapotoa nyimbo.

Rejoice Blog: Ahsante sana Joshua Silomba kwa muda wako, Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu

Joshua Silomba: Amina! Nawashukuru pia Rejoice Blog kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuibua na kutangaza vipaji vya waimbaji wa nyimbo za Injili. Mungu awainue zaidi ili muwafikie watu wengi.


Kupata zaidi habari za huduma yangu kwa sasa natumia Facebook, page yangu natumia jina Joshua Silomba. Msomaji anaweza ku-like na ku-share na wengine ili waweze kujua habari mbalimbali zinazohusu huduma yangu. Pia YouTube kwa sasa nimeweka wimbo (audio) unaoitwa Jambo Jipya wanaweza kuusikiliza kwa kubofya link HAPA

Mawasilianoi zaidi piga: +255717387212/+255754773512

Mwisho kabisa napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa msomaji kutoa muda wake kufuatilia habari za muziki wa Injili kupitia Rejoice Blog.



~~~ UBARIKIWE ~~~