Tuesday, August 26, 2014

Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa -III na Mwalimu Samwel Mkumbo

 

 Mwalimu Samuel Mkumbo pichani
Karibu atika mifululizo yote ya somo hili kutoka mwanzo mpaka sasa imekuwa ni suala la kuangalia ni kwa jinsi gani nafsi zetu zinahusika sana katika Uhai wa Kanisa. Sehemu ya mwisho nitasema nawe kwa kifupi sana kuhusu Uhusiano wa nafsi ya Kanisa.

Karibu tujifunze pamoja…..

Luka 12:15 inasema hivi;

Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

Ni heri kila mmoja akahakikisha ya kwamba Nafsi yake iko na furaha kila wakati, kwa ajili ya uhai wa kanisa lako, lakini pia kwa ajili ya uhai wa nyumba yako kama msingi wa kanisa, kwa ajili ya ofisi yako, kwa ajili ya ukoo wako.

Lakini pia ni vema kila mmoja akahakikisha anafanya bidii kumfurahisha mwingine na kuifanya nafsi ya mwingine isiwe na jeraha hata moja, kuifanya nafsi ya mwingine isitende dhambi, kila mmoja acheze karibu na mwenzake, kama kucheza basi tucheze peke yetu, hakikisha unamlinda mwenzake asipate shida wala asipotee.

1 Wakorintho 8:12 tunasoma hivi;

Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo

Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na

Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa

Sasa labda tutazame kwa nafasi nyingine uhusiano wa Nafsi yako ikiwa na Usalama na ubora wa nafsi yako na Uhai wa Kanisa ikiwa ni la nyumbani au ni mahali unapoabudu au ofisini kwako au hata shuleni kwako unakosoma.

Labda niweke jambo hili la msingi, tunapozungumzia kanisa ni lazima tukajua ya kwamba si suala la dhehebu moja tu au suala la watu wanaosali kwa pamoja lakini suala la Kanisa ni jambo linalohusu watu wote waliookoka na wanaomkubali BWANA YESU kuwa ni mwokozi wa maisha yao na Mfalme wa Ulimwengu wote.

Sasa kuna shida ambayo ni muhimu tukaishughulikia vizuri kidogo ili tusipate shida tunapoangalia utekelezaji wa Somo hili, na jambo lenyewe ni lazima akili zetu na fahamu zetu zifunguke tukajua mambo kadhaa ili tuone Umuhimu wa kuona Nafsi ya kila mmoja inakuwa salama na bora ili Kanisa liweze kuwa Hai.

1 Wakorintho 3:16-17 tunasoma hivi;

Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.

Sasa kuna jambo la msingi hapo natamani tulitazame kwa makini sana sana, maana kama tusipolitazama kwa makini tunaweza tusielewe vizuri, na hilo jambo linatuonesha Uhusiano uliopo kati ya Usalama na Ubora wa Nafsi yako inavyohusiana na Uhai wa Kanisa la Tanzania, Kanisa la Ulimwengu mzima lakini pia kuanzia na Kanisa la Nyumbani kwako na mahali unapoabudu.

Basi tuutazame huo mstari kwa makini sana sana, kuna maneno kadhaa ya huo mstari natamani tuyatazame kwa makini …..Hamjui ya kuwa NINYI mmekuwa hekalu la Mungu….. na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani YENU?....... Kama MTU akiliharibu hekalu la Mungu,… Mungu atamharibu MTU huyo….. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo NINYI.

Maneno niliyoyaweka kwa herufi kubwa yana maana kubwa sana, Paulo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu anawaandikia Wakorintho akitaka kuwaonesha ni jinsi gani Uhusiano wa Kanisa unavyotengenezwa na unavyotegemea mtu mmoja mmoja. Anapozungumzia Hekalu la Mungu anasema ni NINYI au ndilo SISI kama tukijiweka kwenye nafasi ya Wakorintho na ambayo ni nafasi muhimu lazima tujiweke hapo ili hiyo nafasi tuichukue kwa Umuhimu mkubwa sana.

Jambo amabalo ni la kulitazama kwa makini kwenye mistari hiyo ni kwamba inapozungumziwa kanisa basi tunatazama kama Muunganiko wa watu,. Maana HEKALU LA MUNGU (moja) linajengwa na NINYI (wengi), lakini pia inawezekana hilo Hekalu la Mungu ambalo ni watu wengi likaharibiwa na MTU yaani mmoja. Sasa basi kuna jambo la kulitazama tena hapo kwa makini Zaidi, kwamba kama Hekalu la Mungu linalojengwa na SISI linaweza kuharibu na YULE au WEWE basi pia linaweza kujengwa na WEWE- Nitalielezea hilo baadae kwa undani.

Wednesday, August 6, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Usifikiri utaweza kubadilisha tabia ya mwenzi wako baada ya kuolewa naye au Kumuoa

 

Bwana Asifiwe watu wazuri wa Mungu, namshukuru Mungu kwa siku hii nzuri aliyonipa maana kwakweli muda nao umekuwa mali.

Natamani sana kila wiki niendeleze Makala haya lakini mara nyingine tunabanwa na muda lakini pia Mungu ana makusudi kwa kila jambo.

Leo naomba tuzungumze jambo hili muhimu sana katika mahusiano, linalohusu pale mtu anapokuwa na matarajio kwamba mwenzi wake atakuja kubadilika tabia yake mbaya au isiyombariki baada ya kuingia kwenye Ndoa

Hii inakuwa hivi inawezekana watu wamekaa katika uchumba wanavyoendelea kuna tabia unaziona kwa mwenzi wako ambazo unaona kwamba ni ngumu yaani hazibebeki, lakini unaamua kwamba utaendelea maana unajua kwamba ukimuoa au akikuoa utakuwa na Mamlaka ya Kuweza Kumbadilisha au Kukomesha hiyo tabia.

Sisemi kwamba watu wenye udhaifu fulani hawawezi kubadilika,HAPANA mtu yoyote yule anaweza kubadilika ila Mabadiliko yatatokea tu pale mtu ANAAMUA kubadilika na sio kung`ang`anizwa kubadilishwa.

Hakuna aina ya ubabe ambao wewe mke au mume unaweza kutumiakwenye Ndoa ili kubadilisha tabia yake, sio pesa, sio chochote kitakachoweza kubadilisha mtu

Unaweza kuwa na mchumba ambaye ana mahusiano mengi mengi, leo umemkuta na meseji za Joyce, Kesho za Jane,mara umesikia jana alikuwa na mwingine sijui KFC au Steers pale, wengine tena wanakutumia labda meseji za kejeli au wengine wanakupigia simu kwamba huyo ni cha Wote, lakini wewe unang`ang`na kwamba eti huyu mtu wangu atabadilika pale tu Nitakapomuoa….

Kuna kisa nilikisikia hivi karibuni kaka alikuwa mchumba, kumbe huyo dada alikuwa anaendeleza mahusiano ya zamani kisirisiri, sasa kibaya sana siku mbili kabla ya harusi kuna mtu alimuona huyu mwanadada akiwa ametoka kwa yule mtu wake wa zamani, huyu kaka aliambiwa lakini akasema huyo mimi nikimuoa nitamkomesha hataweza kutoka hata ndani nitamfungia, NITAMBADILISHA.

Je Ndugu yangu unafikiri kweli kwa tabia hii huyo dada yetu ataacha mahusiano hayo, kama kweli anashindwa kuheshimu ndoa yake kabla hajaingia maana hapo hata huyo mume hajamjua vizuri je akishaishi naye kweli ndio ataiheshimu hiyo Ndoa. Hebu tafakari hili mpendwa wangu....

Neno katika Mathayo 6: 24“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.”

Ukisoma Maneno ya Mungu hapo juu neno liko wazi Kabisa kwamba mtu huwezi kutumikia mabwana wawili yaani huwezi kushika mambo mawili lazima kuna moja utalidharau na kuzingatia lingine.

Tuesday, August 5, 2014

USALAMA NA UBORA WA NAFSI YAKO UNAVYOHUSIANA NA UHAI WA KANISA na Mwl Samwel Mkumbo -Sehemu ya Kwanza

Karibuni katika makala haya yanayoletwa kwani na Mwalimu Samwel Mkumbo
 
Mwalimu Samwel Mkumbo

Uhai wa kitu chochote kile unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa dhamana yuko katika hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au mambo Fulani lakini kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au aliyekabidhiwa mikononi mwake yuko katika hali gani.

MATENDO 20:28 inasema hivi;

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Sasa kabla sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?

Unaweza usijue wala usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;

KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.

TAZAMA NAMI:

Ili kanisa liwe na Nguvu na likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani ya Kanisa ziwe ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo uhakika wa kundi kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.

Labda tuunganishe vipande viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha kanisa lake Mungu,.,.,..

Mfano wa Mtumwa Mwaminifu

Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini (LUKA 12:42-46)

Sasa hapo ninataka nikufundishe jambo ambalo kimsingi ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu, na lenyewe ni juu ya adhabu aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….

Maana suala sio kusema bwana wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya nini? Na wala sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini? Yeye alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA KULEWA,..,..

Biblia inaposema yeye ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya alichotakiwa kufanya lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa Ulevi. Maana suala si kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa kila mtu, lakini suala ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.