Friday, May 23, 2014

Kutana na Samwel Mwangu mwandishi wa Habari anayemtumikia Mungu kwa njia ya Uimbaji



Samwel Mwangu mwimbaji wa nyimbo za Injili
 
Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.

Mwambaji: Samuel Mwangu

Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi


Mwimbaji: Nimeokoka na ninaabudu katika kanisa la TAG, CITY HARVEST, Dar es salaam.

Blogger Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?

Mwimbaji: Nimezaliwa 1988, katika familia ya kikristo, huduma ya uimbaji nimeanza mwaka 2003 katika kwaya, kanisa la Mission to Unreached church (MUAC), mkoani pwani, mlandizi. Mwaka 2010 Mungu aliniwezesha kuanza kujitegemea katika uimbaji, mpka hivi sasa kwa neema ya Mungu naendelea kutumika.


Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?

Mwimbaji: Mpaka hivi sasa nina albam mbili, ya kwanza inaitwa NINAISHI SABABU YA MUNGU nay a pili inaitwa NJOO VILE ULIVYO ( UTAN’GAA KAMA JUA.)

 
Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo zako

Mwimbaji: NJOO VILE ULIVYO ninaupenda zaidi.


Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo

Mwimbaji: Kwa sababu unaelezea zaidi juu ya pendo la yesu katika maisha yetu wanadamu, pia biti ya wimbo huu na mpangilio wa maneno yake ni nzuri mno.

Blogger:Nani anasambaza kazi zako? Je anakusaidia vizuri?

Mwimbaji: Kwa sasa nasambaza mwenyewe, bado sijafanikiwa kupata msambazaji.


Samwel Mwangu akiwa katika utumishi wa Kumuimbia Mungu
 
Blogger:Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili

Mwimbaji: Mafanikio sio makubwa kwa sasa, kwani bado sijapata soko la kuuza kazi yangu, na pi bado sijafanya promo ya kutosha.

Blogger:Umekutana na changamoto gani katika safari yako ya kuimba

Mwimbaji: Changamoto kubwa ni swala la fedha, imekuwa ni kikwazo kikubwa kwangu. Na pia kupata msambazaji.

 
Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?

Mwimbaji: Music wa injili Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa sana, ila soko bado lipo chini, wizi wa kazi za wasanii umekuwa mkubwa sana, watu wanachukulia kawaida.

 
Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii

Mwimbaji: Wito wangu kwa waimbaji ni kutunza maisha yao, wajali utakatifu wasiondoe uthamani wao kwa sababu ya changamoto wanazopitia, iwe  ni binti ua kijana wa kiume.waishi maisha ya mfano, ili Mungu ajitukuze katika maisha yao.


Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya

Mwimbaji: Ni mwandishi wa habari

Blogger:Je kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado? Watoto wangapi?

Mwimbaji:Bado sijaoa, ninaishi mwenyewe hapa Dar es salaam.



Hata Kinanda anapiga
Blogger:Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania

Mwimbaji: Wasikate tama katka kutumika, wamtangulize MUNGU mbele zaidi kuliko PESA.

Blogger: Una Ujumbe gani kwa Jamii inayoburidishwa na nyimbo za Injili

Mwimbaji: Waendelee kutusupport kwa kununua  kazi zetu.

Blogger:Asante sana kwa Muda wako,Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu.Amen

 

Mwimbaji :Asante sana kwa ushirikiano wako.
 
Amina Ubarikiwe Samwel, ukitaka kumkaribisha kwa huduma yuko tayari kabisa tuwasiliane, Haleluya



 

No comments:

Post a Comment