Tuesday, October 22, 2013

Utawala wa Fedha na Mchungaji Jeremiah –TAG Makoka


Hili Somo limenibariki sana naomba na Mungu aseme na wewe unaposoma Somo hili muhimu


Specimen
 

Luka 16: 1-13 “Akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na meneja wake. Ilisemekana kwamba huyo meneja alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. 2 Basi huyo tajiri akamwita meneja wake akamwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayosikia kukuhusu? Nitay arishie hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu kwa maana hutaendelea kuwa meneja tena.’

 

3 “Yule meneja akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu anataka kuniondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, na ninaona aibu kuombaomba! 4 Najua nitakalofanya ili nikipoteza kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’

 

5 “Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa tajiri wake, mmoja mmoja. Akamwuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ 6 Akajibu, ‘Galoni mia nane za mafuta ya alizeti.’ Meneja akamwambia, ‘Chukua hati hii ya deni lako, ibadilishe upesi, uan dike mia nne.’ 7 Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’

 

8 “Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko watu wa nuru kukamilisha mambo yao. 9 Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.

 

10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”

Katika mstari hapo juu Bwana Yesu anazungumza na wanafunzi wake kama alivyokwisha kuzungumza na Petro katika Mathayo 16:13 -18 “13 Basi Yesu alipofika katika wilaya ya Kaisaria Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu husema mimi Mwana wa Adamu kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya; na wengine husema kwamba ni Yeremia au mmo jawapo wa manabii.” 15 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

17 Na Yesu akamwambia, “Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwanadamu aliyekufunulia hili, bali ni Baba yangu aliye mbinguni. 18 “Nami nakuambia, wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lo lo te utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

Bwana Yesu anataka kujenga Kanisa lake na milango ya Kuzimu haitalishinda.

Kanisa ni mtu anayemwamini Kiristo yaani mimi na wewe.

Kuweza kushinda milango ya kuzimu lazima Mkiristo aweze pia  kuwa na Utawala wa fedha, kama ilovyoandikwa katika mstari wa Luka 16:1-13 hapo juu.

Tajiri amesikia kwamba wakili anatapanya mali, akamwambia wakili atoe hesabu na atamnyang`nya uwakili.

Wakili dhalimu akakumbuka kwamba Bwana wake amekopesha watu kwa riba ambacho ni kinyume na Torati, akawaita akawapunguzia madeni yao ili aweke urafiki nao maana ameona kwamba kazi yake ya uwakili inaondoka.

Bwana anategemea amtumie Mwamini alihudumie kanisa kwa utawala wa fesha kama vile kutoa Zaka na sadaka nyingine.

Vitu muhimu vya kujifunza katika Neno hili:


1.      Mwamini anatawala fedha lakini sio za kwake, Mali zote ulizonazo umepewa uzitawale lakini ni za Mungu sio za Kwako. Wakili alikuwa anatawala mali za Bwana wake hazikuwa za kwake. Kwa yule aliye katika sharia fungu la kumi tu ndio la Bwana lakini sisi tulio katika neema vyote tulivyonavyo ni mali ya Bwana, Vyote ni vya Mungu.

Je Mpendwa uko chini Neema basi kama uko chini ya Neema vyote ulivyonavyo ni vya Bwana ameweka tu mikononi mwako, Vitu hivyo ni kama Mali, Watoto,Wakati , fedha nakadhalika

Kumbukumbu la Totati 6:7 “nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.”

Watoto: Hata watoto wetu tumepewa kama Zawadi tu tuwalee kama Mungu anavyotaka

Wakati: Siku ya hukumu utatoa hesabu jinsi ulivyotumia wakati wako je ulitumia kwa ajili ya Bwana au kwa ajili yako mwenyewe?

Mali na Fedha: Tutatoa hesabu jinsi tulivyozitumia je tulitumia katika kazi ya Bwana au mambo yetu wenyewe

1 Wakorintho 13:2 “Na ikiwa nina zawadi ya kutoa unabii+ nami nazijua siri takatifu+ zote na ujuzi+ wote, na ikiwa nina imani yote kuweza kuhamisha milima,+ lakini sina upendo, mimi si kitu.”

Sisi ni watumwa wa Upendo, ina maana unaweza kuwa katika ngazi ya juu sana kama Nabii anayefundisha kwa ufasaha sana lakini kama huna upendo ni kazi bure. Au mtu ana dhahada ya Uzamivu katika mambo ya Theologia lakini kama hana upendo ni kazi bure.

Na njia mojawapo ya kuonyesha upendo ni jinsi tunavyotawala fedha tulizopewa na Bwana kwa kutumia katika kazi ya Bwana.

 

 

 

2.      Utoaji wa Fungu la Kumi ni wajibu wa Kila Mkristo mwamini na litolewe kwa uaminifu.

Hiyo sio ya kwako unatakiwa utoe kwa Uaminifu, Ili tujenge Kanisa la Kristo jambo la Kiroho ni kutoa fungu la Kumi kwa Uaminifu.

Hizo 9 ya kumi zilizobaki bado sio za kwetu tunakuwa nazo tu ili tuzitawale tumepewa uwakili bado ni mali ya Bwana, kwahiyo unatakiwa umuulize Mungu akuongoze jinsi utakavyozitumia na akuonyeshe mapenzi yake nini. Maana hata hizo zilizobaki haziwezi kutosheleza mahitaji yetu ya kila siku ila tukimkabidhi Bwana atuongoze yeye atatoa katika hazina yake kukutana na mahitaji yetu na tutakuwa na maisha ambayo hatuishi kwa hofu.

Neno la Mungu katika Wafilipi 4:19 “Na Mungu wangu atawapeni ninyi kila kitu mnachohitaji kwa kadiri ya uta jiri wake mtukufu katika Kristo Yesu”

Hatuishi kwa hofu juu ya maisha haya Bwana atashughulika na mahitaji yetu kama neno lake linavyosema hapo juu.

Tusiwe na hofu kwa kuzuia fedha kufanya kazi ya Bwana maana atatujaza kadiri ya utajiri wake.

Mali tuliyonayo inatusiaidia kuwa na hazina mbinguni, tuweke hazina Mbinguni

 

 

3.      Mwamini anatakiwa kuwa mwaminifu kwa kidogo au kingi alichonacho

Waamini wengi wanachukia kutoa zaka hadi wanakuwa na maandiko ya kuwatia moto wasitoe zaka kwasababu hawajajifunza kuishi kwa upendo.

Yakobo 5:3 “Dhahabu yenu na fedha yenu vimeingia kutu na kutu yake itakuwa ushahidi dhidi yenu na itakula miili yenu kama moto. Mmejilimbikizia utajiri kwa siku za mwisho.”

 

Watu wenye mali nyinge wanaona wakitoa fungu la kumi kubwa ni jingi sana kwa kanisa.

Na wenye mali kidogo wanaona hawana kitu cha kumtolea Bwana na wakitoa watabaki masikini.

Hoja zote hizi zinaonyesha moyo wa mtu na mahusiano na Mungu, Kwasababu mahusiano yakiwa mazuri mtu atatoa kwa upendo.

Hatutakiwi kuzipenda fedha hadi zikatutawala bali tunahitajika kuishi kwa Utaua na kuzitawala Fedha.

1 Timotheo 6:10 “Maana kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote. Tamaa ya fedha imewafanya wengine watangetange mbali na imani na kuteseka kwa huzuni nyingi”

 

Mithali 3: 9-10 “Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.”

 

Tunatawala fedha kwa ajili ya wakati ujao, Mali nyinge au Kidogo sio sababu ya kutotoa Zaka, kuwabariki masikini na wenye uhitaji mbalimbali.

Vitu vyote Mungu alivyokupa ni kwaajili ya Kujenga Ufalme wa Mungu,vitu kama Elimu, Hekima, Ujuzi vitumie pia kuujenga ufalme wa Mungu.

 

Kumbukumbu la Torati 16: 17 “Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya Bwana, Mungu wako, alivyokupa”

 

 

 

No comments:

Post a Comment