Wednesday, October 23, 2013

Uchumba hadi Ndoa: Hakikisha Mwenzi wako anajali Malengo na Ndoto zako


 

Karibu katika somo hili la Uchumba hadi ndoa, kama wewe ni mgeni katika masomo haya karibu sana naomba upitie katika mtiririko wa masomo ya nyuma utajifunza mambo mengi ya muhimu.

Leo naleta kwenu somo hili muhimu la umuhimu wa kuhakikisha mwenzi wako anajali malengo na ndoto zako.

Kabla hujaoa au hujaolewa ulikuwa na malengo na ndoto zako za maisha kwamba unaona kabisa Mungu amekuita uwe labda Mchungaji, Mmishionari, Mwinjilisti,Mfanyabiashara,Mkulima,Mshauri nakadhalika nakadhalika, sasa hayo maono yako ndio huduma yako ambayo umeitiwa na Mungu hapa duniani kwahiyo huna budi kuyafikia. Utauliza mfanyabishara inawezaje kuwa wito, ni wito kabisa maana unatoa huduma kwa jamii kwasababu usipotengeneza unga wa ugali Mungu atakuuliza niliweka maono hayo ndani yako watu wamekufa na njaa kwasababu hukufanya sehemu yako.

Au jamii ikakosa nguo za kujisitiri hautajisikia vizuri kwasababu unajua kabisa hapa nilipaswa nihudumie jamii kwa huduma ya kuuza nguo.

Kila shughuli Halali ambayo Mwanadamu anaifanya inakuwa na Baraka za Mungu maana hata tukiangalia katika Biblia watu walikuwa na Shughuli mbalimbali tumchukue Petro Yesu alimkuta katika shughuli zake za Uvuvi wa Samaki ndipo akamwambia amfuate atamfanya mvuvi wa watu.

Pia kama mtu umeitwa kuwa Mchungaji, Nabii, Mtume au Mshauri usipofanya ujue kuna watu wakifa bado hawajampokea Kristo utakwenda kuulizwa kwanini kuhumuhubiria, au mtu akakata tamaa akajiua utaulizwa kwanini hukumtia moyo wewe mshauri.

Kwahiyo Malengo na Ndoto zako ambazo unazo ziheshimu sana sanaa kwasababu sio mtu au mkuu wa ukoo wenu, bibi, babu yako ameweka ndani ya ni Mungu amekubariki nazo, kwasababu hiyo angependa kuona zinatimia bila kutoa sababu yoyote, anakudai.

Unapokuwa umepata mwezi wa maisha mshirikishe ndoto zako ili ajue yuko na mtu wa aina gani na wewe utapata nafasi ya kujua mawazo yako juu ya hizo ndoto kwamba anazijali au ataziua.

Kuna mpendwa alimshirikisha mwezi wake ndoto zake wakiwa tu katika hatua ya uchumba akamwambia nina ndoto ya kuwa kitu fulani kwahiyo inanilazimu nikasomee Shahada ya Uzamili, yaani yule mwezi alikuja juu akasema mimi sitaki kabisa mke mwenye kusoma soma na kufanya shughuli shughuli nataka akae nyumbani aangalie watoto na nyumba yaani ikawa kasheshe kweli. Sijui waliishia wapi ila yule dada yeye alikuwa na ndoto na huyu mwezi hakuijali kwasababu yeye alikuwa na matakwa yake, labda yule dada yeye angekuwa na ndoto ya kutofanya chochote nafikiri isingekuwa tatizo lakini alikuwa na ndoto.


Huo mfano inaonyesha kwamba kama wako pamoja lazima kuna ndoto zimeuwawa hapo kwahiyo huyo dada anadeni kwasababu hajafanya wajibu wake Mungu aliomwitia.

Vilevile kama una mwenzi ambaye haamini Imani yako saa nyngine anaweza asiamini malengo na ndoto yako kwasababu hivyo vinakuwa vimechochewa na kile unachokiamini  sasa kama yeye anaamini tofauti na wewe hataruhusu zitimie. Na ndio maana neno linatuasa katika 1 Wakoritho 6:14 “Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?” Usije ukaambatana na mtu asiamini kwasababu wema na uovu au mwanga na giza haviwezi kukaa pamoja.

Kile unachoamini wewe ni mwanga lakini kwa vile yeye yuko gizani anaweza asikijali ukajikuta haufanyi lile kusudi Mungu alilokuwekea hapa duniani, Haleluyaa
Mwenzi mwingine anaweza asijali malengo na ndoto yako kwasababu anaona unafanya tu vitu lakini hujamshirikisha, hebu leo chukua hatua mshirikishe afahamu nini kinakukosesha usingizi je una wito wa kuwa mwanasiasa ili upiganie haki za nchi yako mwambie tu maana ukikurupuka ndipo hapo atakuzuia utabaki ukilalamika. Hii sio kwa wachumba tu hata WANANDOA shirikishaneni nini malengo na ndoto zenu.

 

Umuhimu wa Kumshirikisha Mwezi ndoto zako:

1.         Utaweza kujua kwamba uko na mtu ambaye anajali na atakupeleka katika malengo yako au   atakayeyaua

2.         Kama anajali malengo yako basi ataweza kukushauri hata jinsi ya kuboresha zaidi hayo malengo na ndoto

3.         Atakuombea kama anajali hayo malengo na ndoto zako

4.         Atakupa uhuru wa kufanya shughuli mbalimbali zinazohusika na kufanya malengo na ndoto zako zitimie kama vile kwenda semina na warsha mbalimbali

5.         Utafikia malengo na ndoto yako kwa furaha kwasababu unajua yuko mpenzi wako anayeyajali pia

6.         Utakuwa huru kufanya shughuli zinazohusika na malengo na ndoto yako kwasababu mwenzako anajua , huna haja ya kuficha ficha vitu kusema uongo ili kukwepesha kujulikana kile unafanya

Inawezekana uko katika mahusiano na tayari huyo mwenzi anaonyesha dalili ya kutojali kabisa malengo yako, hebu liweke katika maombi na ujichunguze je umemshirikisha na sababu za kuzuia ni nini woga au labda anahofia washirika wako wa kuelekea hiyo ndoto? Kama washirika hawambariki tafuta kwanini labda mko karibu kuliko yeye? Kama ndio katika haya badili jinsi unavyoenda ili aridhike, ILA kama anakataa tu kwasababu yeye hataki ufanye chochote kile endelea kuomba Mapenzi ya Mungu juu ya hilo Bwana atafanya njia na kama sio wako utashangaa tu anajiondokea taratiibu.

 

Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog Mengi Mazuri yanafanya, kama tunavyojua hii ni Zaidi ya Blog

 

BARIKIWAAA

No comments:

Post a Comment