Wednesday, May 15, 2013

Vijana wa Tanzania washauriwa kuwa na Fikra Kubwa ili kuleta maendeleo katika nchi yao


Profesa Elisante Ole Gabriel Mkurugenzi Mkuu Idara ya Mendeleo ya Vijana Tanzania
Maneno hayo yalisemwa na Profesa Elisante Ole Gabriel ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa maendeleao ya Vijana katika Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo alipokuwa anaeleza Vijana juu ya Sera ya Maendeleo ya Vijana katika Ukumbi wa Nchi ya Ahadi ( The Promise Land). Semina hiyo ni mojawapo ya semina na mikutano ambayo imekuwa ikifanyika katika ukumbi huo kila wiki ili kuhamasisha vijana watanzania waweze kubadili mtazamo na kuikwamua nchi yao,mikutano hiyo inaandaliwa na Mchungaji, MC Maarufu na Mtangazaji wa Redio Clouds FM Harris Kapiga.

Katika mkutano huo Profesa Elisante aliwataka vijana wa kitanzania kuachana na dhana potofu kwamba maendeleo yanahitaji kuwa na mtaji au hela tu wakati tatizo kubwa liko katika fikra na mtazamo wa vijana kwa ujumla.

Aliendelea kusema kwamba wameweza kugundua kwamba vijana watanzania wanakabiliana na changamoto kuu nne; ambazo ni

·         Fikra,kwamba kuna watu wenye fikra Kubwa,fikra ya wastani na fikra ndogo

Ili kujikwamua ni lazima vijana waamue kuwa na fikra Kubwa.

·         Uelewa wa kuongeza thamani katika shughuli za Uzalishaji Mali (Value Addition)

·         Upatikanaji wa Mtaji kwa gharama nafuu

·         Mifumo ya kiutendaji kama leseni,lugha,rushwa e.t.c

Pia aliweza kuelezea jinsi ambavyo serikali imefanya jitihada kubwa kuweza kupambana na changamoto hizo;

·         Kuanzisha kanzidata ya taarifa za Vijana ili kujua takwimu ya vijana ikoje,kwa mfano wangapi wana kazi wangapi hawana

·         Kuzungumza na Taasisi za fedha ili kupata mikopo ya gharama nafuu

·         Kuimarisha mfuko wa maendeleo ya vijana ili kuwezesha vijana kupata mikopo ya vikundi kwa gharama nafuu

 

Alielezea pia mambo ya msingi kwa vijana yanayoweza kuwezesha Sera ya Maendeleao ya Vijana kutekelezeka kwa urahisi

·         Vijana wasibaguane kwa rangi,dini,siasa,jinsia,jiografia,elimu,kipato au tofauti yoyote ile

·         Kijana awe na itikadi ya dini na siasa ila ujana wako usiwe na itikadi

·         Vijana wafanye kazi kuanzia asubuhi,hapa akasema tatizo vijana wengi wanalala sana

·         Kila mtu ahuheshimu ujana wako,pia wewe ujiheshimu ili uheshimiwe

 
Harris Kapiga Mchungaji,Mc na Mtangazaji mwenye mzigo na Vijana wa Ktanzania


Kwa kweli semina hiyo ilikuwa nzuri sana iliweza kuwafungua vijana kujua hata fursa ambazo wanazo kupitia wizara yao. Na vijana waliweza kuuliza maswali na kupatiwa majibu pia hata sehemu za kupata huduma katika wilaya zao.

 

Vijana walifurahishwa sana na jinsi Prof Elisante alivyotumia muda wake na kueleza kwa kina na hata akitumia mifano ya maisha yake hadi hapo alipofika aliwapa vijana changamoto ya kujituma zaidi na zaidi.

 

Blog inamshukuru sana Profesa Elisante kwa alivyojitoa kwa vijana na pia inampongeza sana Harris Kapiga kwa mbegu anayoipanda kwa Vijana wa kitanzania,hasa ile passion aliyo nayo kwamba Kijana wa Tanzania inawezekana hata kama uko stage gani.

 

No comments:

Post a Comment