Tuesday, February 5, 2013

MAOMBI NDANI MWA MAOMBI NA MCHUNGAJI FLORIAN KATUNZI


KILA PANDO ASILOLIPANDA MUNGU LITANG’OLEWA



Rev Florian Katunzi
Karibu katika makala haya yanayoandaliwa na hufundishwa na Mchungaji Florian J. Katunzi, wa kanisa la EAGT City Centre, lenye makao yake viwanja vya Mwal. Julius Kambara Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Wiki hii tutaanza na Somo Maombi ndani mwa maombi, katika kipengele kinachosema… “Kila pando asilolipanda Mungu  litang’olewa.”. Endelea…….

Ndugu zangu tuliolipokea Neno, BWANA ametuita tuisikie sauti yake na kutii agizo lake, andiko lifuatalo linatuelekezaq jukumu tunalopaswa kufanya. Hebu msikie: Lakini lisikieni Neno la BWANA, enyi wanawake, enyi wanaume, na masikio yenu yapokee Neno la kinywa cha Mungu.( Yeremia 9:20-21).



Mkafundishe binti zenu, vijana wenu kuomboleza na kila mtu mmoja na jirani yake. Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, ipate kuwakalia mbali watoto wetu na vijana katika njia kuu, kazi ya mikono na shoka mapanga na mawe. Yatupasa tusimame tuzifishe roho hizi na kuzing’oa kila pando asilolipanda Mungu wetu. Maombi hugeuza hali ya muombaji, ndani mwa maombi hali zote mbaya zitageuzwa kuwa njema.
Katika Zaburi 46:1-11 Neno linasema: “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaad utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari….BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, … atavikomesha vita hata mwisho wa dunia; avunja uta, akata mkuki…”
 Usiogope jipange katika safu za maombi ya kufunga majibu yetu yatakuwa dhahiri mbele zetu, hapana mapando yatakayosalia. Sauti ya Mungu katika Zaburi 50:15 inasema: “Ukaniite siku ya mateso; nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”Tena kwenye Zaburi 55:22 inasema “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe
 milele.” Maana adui zetu wanataka kutumeza, maana waletao vita juu yetu kwa kiburi ni wengi, lakini kwa msaada wa Mungu wataanguka hawatasimama tena.Kwa msaada wa Mungu watarudishwa nyuma hawatainuka tena.BWANA ananena katika Zaburi 55:16-18; “Nami
nitamwita Mungu, na BWANA taniokoa; jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu, Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu, maana
walioshindana nami walikuwa wengi.”Tukiomba Mungu atalilinda kanisa letu la Tanzania.
 • Mkiomba Mungu atalinda nchi yetu na
   kuiponya.

• Nafsi zetu zitaokolewa, nafsi za watanzania zitakuwa salama. Na maadui wa nchi yetu; hawatasimama tena maana BWANA anasema: “Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai, maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.” (Zaburi 55:15). Kila pando asilolipanda BWANA lazima leng’olewe kwa njia ya maombi. Ndani mwa maombi tutamwambia Mungu tukisema achafue ndimi zao wakwaruzane. Katika Zaburi 55:9 Neno linasema: “Ee BWANA, uwaangamize, uzichafue ndimi zao, maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.”
Huu ni wakati wa kuyang’oa yalipandwa kinyume, haya ndiyo maombi ya siku ishirini na moja tuliyoomba na yamekuwa sababisho la baraka zako na kuinuliwa tena.

• Sababisho la ndoa yako kustawi tena.
• Ni maombi yenye kufungua malango yaliyofungwa.
• Ni maombi yenye sababisho la kibali chako.Yesu anasema: “Amin, nawaambieni, yoyote         mtakayofunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayofungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” (Mathayo 18:18).
Ndani mwa maombi tutafungwa makanwa yote ya mauti na kuzimu kama alivyofanya Danieli, tutaizimisha nguvu ya mwili, (Daniel 6:1-28).

Mungu aliyetuma malaika kuifunga mauti na uaribifu usimpate Danieli aliyemtumaini Mungu kwa maombi ndiye Mungu tunayemtumikia na mamlaka yake ni yale yele hajabadilika. Pamoja na waraka wa kifo kutiwa saini Danieli nakuacha kuomba, bali alidumu ndani mwa maombi kama alivyokuwa akifanya, hapo kabla ya kuinukiwa na watu wabaya.
Nasi tusitoke katika msingi wetu wa maombi, tukaacha kuomba na kuanza kubeba majambia, kufanya hivyo tutaivuruga nchi yetu na kuibomoa kwa mikono yetu; Bali tuombe na kuwa macho
kwa jinsi ya rohoni, ndani mwa maombi, Mungu atageuza
uteka wetu juu ya adui wainukao kinyume na ustawi wako na familia yako.
 Katika maombi tunashinda na zaidi ya kushinda katika yeye atutiaye nguvu.
 Mdo 12:1 Tunasoma na kuona aalivyoinuka Herode kuwatenda mabaya watu wakanisa. BWANA hataacha wateule wake wapate uaribifu. “Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitakaribia hema yako.

”(Zaburi 91:10).Maandiko pia yanatuambia: “Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia” Katika Zaburi 34:6 pia tunasoma: “Maskini huyu aliita,BWANA akasikia, akamwokoa na taabu zake zote.”
BWANA atawavunja maadui zetu na kuwang’oa.
Zaburi 28:5 “Maana hawazifahamu kazi za BWANA, wala matendo ya mikono yake. Atawavunja wala hatawajenga.” Pia katika Yer 9:17-21. Andiko linatuambia:  “BWANA wa majeshi asema hivi, fikirini ninyi,mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake
wenye stadi, ili waje, na wafanye haraka na kutuombolezea,ila macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujika maji”Kwa maana mauti imepanda madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu


Tuendelee wiki Ijayo siku kama ya leo

1 comment:

  1. Amina mtumishi,asante sana kwa kutufundisha umuhimu wa maombi

    ReplyDelete