Tuesday, January 29, 2013

AFLEWO (Africa Lets Worship) Tanzania 2013 kutikisa jiji la Dar es Salaam



Waimbaji wakiendelea na mazoezi

Maandalizi ya AFLEWO Tanzania yanaendelea vizuri sana,weekend hii nilipata nafasi ya kuhudhuria katika mazoezi waliyokuwa wakiyafanyia katika kanisa la World Alive,Sinza.

Wakienda sawa chini ya uongozi wa Music Director Pastor Sam
 
Pia nilifanikiwa kuongea na Mwenyekiti wa maandalizi aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Geoffrey Obiero,akisema kwa sasa wamepata waimbaji wengi sana ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo kwasasa wamepata waimbaji kutoka makanisa 32 ya hapa Dar es Salaam. Kwa mahesabu ya harakaraha yawezekana wakapata waimbaji takriban 50 kama trend itakwenda kama ilivyo.





 

Kwa kifupi aliniambia AFLEWO ni kifupi cha “Africa Lets Worship”,ambayo ilianzia Nairobi nchini Kenya ,na ina maono kuwa na usiku mmoja wa Kuomba,Kusifu na Kuabudu katika Africa ifikapo mwaka 2017. Na maono haya yanaonekana yatafikiwa maana nchi nyingi sana zimeshaanza AFLEWO na nyingine zinaendelea kujiunga.

Kwa Tanzania AFLEWO ina walezi watatu (3) ambao ni Bishop Deo Lubala,Pastor Abel Orgenes na Pastor Paul Safari.

Wanategemea kuanzisha katika miji mingine kama Zanzibar,Moshi,Mwanza na kwingine kama mambo yataenda kama walivyopanga.

Music Director akiongoza kwa vitendo hapa si mwingine ni Pastor Sam

 

Mwaka uliopita AFLEWO ilifanyikia CCC-Upanga na ilihudhuria na watu takriba elfu sita(6000). Mwaka huu itafanyikiwa BCIC Mbezi Beach kwa Mchungaji Gamanywa na wategemea kuwa na watu kama elfu 10 hivi.

Mwenyekiti wa maandalizi anawaomba watu wawe tayari kupokea watakapokuwa wanamwabudu na kumsifu Mungu siku hiyo maana inakuwa ni siku ya kuimba bila kukaa na itakuwa ni kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 asubuhi,Wooow je mpendwa utatoka kweli pale kama ulivyoingia jibu ni hapana,jiandae basi maana muda bado upo wakujiandaa na kizuri zaidi HAKUNA KIINGILIO.

AFLEWO 2013 Tanzania itafanyika tarehe 3 mwezi wa tano mwaka huu.

Kwakweli waimbaji hao wamejitoa sanasana  ili tu  kuifanya siku hiyo iwe ya kipekee ya kumwinua Mungu kwa njia ya Kuabudu na Kusifu,maana nimeambiwa kwamba wanafanya mazoezi kuanzia masaa 8 hadi 10 kwa siku,huko ni kujitoa kwa hali ya juu ambapo kama kuna mtu amejisajili katika kikundi hicho na huduma ya kusifu na kuabudu haiku ndani yake atafika kipindi atakimbia tu.
Wakimsikiliza Music Director kwa makini

Niliweza kuona waimbaji kutoka vikundi na makanisa mbalimbali wakiwa ni mojawapo ya kikundi cha AFLEWO Tanzania 2013. Upande wa Vyombo nilimuona mtumishi mmoja ninayemuheshimu sana katika upigaji wa Gitaa,yaani hiyo tu inaonyesha kwamba AFLEWO Tanzania 2013 haitakuwa ya kawaida.

Nikamuona Music Director wa AFLEWO Tanzania 2013 Pastor Sam akifanya kazi yake kwa juhudi kubwa tena bila kuchoka ili tu kuhakikisha kwamba AFLEWO Tz 2013 inajiweka vizuri ili siku hiyo watu wafunikwe na wingu la utukufu kutoka Mbinguni . Maana tunajua neon linasema Mungu hushuka katika sifa.

Mazoezi yao si ya sauti tu na viungo kidogo ili kujenga staminina,kwakweli wanafanya kazi nzuri sanaa.
Waimbaji wakifanya mazoezi ya viungo pia kujimaarisha zaidi
 

WOTE MNAKARIBISHWA na tuendelee kuombea maandalizi

 

.
 

No comments:

Post a Comment