Friday, January 20, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 20

SIKU YA 20 - 20/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUYAKABILI MAMBO YA SIRI/ATTACKING BEHIND THE SCENE

UNITAKASE NA MAMBO YA SIRI.

Changamoto ya watu wengi ni kuishi vizuri nyuma ya pazia wakati hakuna mtu anayemuona, je umewahi kumuona mtu kabla hajatupa uchafu barabarani anaangalia kwanza ni nani anamuona? KUNA TATIZO mahali…

Hata kama hakuna mtu anayekuona uwe na uhakika Mungu anakuona…. UKIWEZA KUSHINDA UBAYA NYUMA YA PAZIA Ni rahisi kushinda mbele ya kadamnasi…. Ukiingia leo makanisani watu wamebandika BIG G au Bubblish kwenye viti kwa siri bila mtu yeyote kuwaona… HUU NI UGONJWA…. CHARACTER PROBLEM.. Kufanya jambo baya kwa sababu hakuna anayekuona ni hatari sana…

Changamoto ni kwamba MUNGU Huvumbua mambo ya siri tokea gizani, Na hicho kilicho giza tupu huleta mwangani Ayubu 12:22

UKIONA YAMEANDIKWA UJUE YALIVUJA….

2 Wafalme 17:9 Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.

LAKINI PIA MUNGU HUZILETA HUKUMUNI SIRI ZA WANADAMU…


Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.

SIYO MATENDO TU HATA MANENO YALIYOSEMWA SIRINI…

Mhubiri 12:14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Lakini Luka 12:3 Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.

NA NDIO MAANA DAUDI AKAONA ASHUGHULIKIE MAMBO YA SIRI…..

Zaburi 19:12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.

NI VYEMA KUMHESHIMU MUNGU NA KUTENDA WEMA SIRINI NA MWANGANI, USIKU NA MCHANA…KATIKA HALI ZOTE…

MAMBO YAKO YA SIRI YAKIWEKWA WAZI UTAKUWA WA KWANZA KUANGALIA?? KAMA SIVYO… MUOMBE MUNGU AKUTAKASE NA MAMBO YA SIRI SASA NA HATA MILELE….

IKIWA UNATAKA KUFIKA MBALI KWENYE HATIMA YAKO… CHANGAMKIA HILI DILI… Ee BWANA Unitakase na mambo ya siri

ATTACKING YOUR BEHIND THE SCENE WHERE NOBODY SEES…

TUOMBE

Ee BWANA Unitakase na mambo ya siri. Uniepushe na ukaidi ninaujua ambao watu hawajui.. nisikutende dhambi eti kwa sababu hakuna anayeniona. Nisipite njia ya mataifa eti kwa kuwa wenzangu hawapo karibu. Ninaomba niwe mtu wa adili maana Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. (Zaburi 112:4). Mimi ni nuru ya ulimwengu Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza (Yohana 1:5). KILA JAMBO NITAKALOLIFANYA NYUMA YA PAZIA LITAENDANA SAWA SAWA NA MAAGIZO NA UKWELI WA NENO LA MUNGU… Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. (Zaburi 19:14)

NIMEJIEPUSHA NA MAMBO YA SIRI YASIYOLETA UTUKUFU KATIKA JINA LA YESU………..

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 NITATEMBEA NURUNI

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

Thursday, January 19, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 19

SIKU YA 19 - 19/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

2017 KOMBOA WAKATI NA KUPINGA WANAOKULA MUDA WAKO

NZIGE, NA PARARE, NA MADUMADU, NA TUNUTU, JESHI KUBWA LILILOKULA MUDA WAKO… mwaka 2016 

LAKINI NAJUA UNAWEZA KUKOMBOA… Waefeso 5:16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

NA BWANA ANAWEZA KUKURUDISHIA Yoeli 2:25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

HILI SIYO SUALA LA UMRI ULIOPOTEA BALI NI MATOKEO YA KAZI ILIYOFANYIKA AMBAYO HAIONEKANI….. Mithali 14:23 Katika kila kazi mna faida; I WAPI FAIDA YA KAZI ZAKO??...

Yoeli 1:2-4 Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu? Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine. Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.

UKISOMA MISTARI YA CHINI UTAGUNDUA KUNA VITU VINGI VIMEHARIBIWA Yoeli 1:7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe. ANGALIA TENA Yoeli 1:17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka. ALIPOFIKA MLANGO WA PILI BAADA YA KUMLILIA BWANA Yoeli 1:19 Ee Bwana, nakulilia wewe; Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani, Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.

HAYA NDIYO MAJIBU YAKE…. Yoeli 2:25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

JE, WATARUDISHIWA 2015 AU 2014? HAPANA… NI NGUVU KAZI ILIYOPOTEA
REDEMPTION/RECLAMATION/RESTORATION…

Kwa mfano: Kama ulitakiwa leo….uwe na nyumba na bado huna… na kujenga kikawaida hutumia miezi 6 REDEMPTION hukufanya urudishie kwa speed NYUMBA na vitu ambavyo unatakiwa kuwa nazo leo….ambavyo ADUI ALIZIHARIBU AU KUZIBANIA…

MFANO MWINGINE.. Kama leo ungezaa mtoto mmoja mmoja ulitakiwa kuwa na watoto watatu… REDEMPTION hukupatia MAPACHA WATATU (TRIPLETS) 

Hapa wale ulioanza nao halafu ulipopotea wakakuacha huwa wanajiuliza, kha mbona juzi tu ndo kaanza? 

HAPA SIO KURUDISHIWA SIKU BALI PRODUCTIVITY (MAZAO) YA SIKU ZAKO ZILIZOPOTEA.. 

UKIMUOMBA MUNGU AKOMBOE VITU VYAKO, HIVYO NDIVYO ZITAKAVYOFANYIKA IN JESUS NAME

*NAPINGANA NA KILA JAMBO LINALOWEZA KULA UWEZO WANGU WA KUZALISHA KATIKA JINA LA YESU, NAKOMBOA VYOTE NILIVYOPOTEZA KATIKA JINA LA YESU, NACHUKUA SPEED SAWA SAWA NA NILIVYOPOTEZA KATIKA JINA LA YESU… KILA ZAO LANGU LA HAKI LINANIRUDIA… SITAPOTEZA TENA KATIKA JINA LA YESU*

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 KOMBOA WAKATI NA KUPINGA WANAOKULA MUDA WAKO


SASA OMBA KWA MANENO YAKO

KAMA UNA TATIZO KUMALIZA SIKU HALAFU UNASHANGAA HAKUNA IMPACT YOYOTE YAANI KAMA VILE ULIRUKA SIKU HIYO…OMBA, KEMEA, PANGA MUDA WAKO VIZURI, ANGALIA MUDA WAKO UNAVYOTUMIKA ILI USIPOTEZE TENA, ACHANA NA MAMBO YASIYO NA MBELE WALA NYUMA

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Wednesday, January 18, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 18

SIKU YA 18 - 18/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KULINDWA DHIDI YA MAGONJWA NA UDHAIFU WA KILA NAMNA

Kati ya mambo ambayo Yesu aliyabeba msalabani ni magonjwa na udhaifu wa kila namna, iliyokuwa imestahili kuwa yetu.

Isaya 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu, Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona

Mathayo 8:17 .....Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

Mathayo 4:23......na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna.

Magonjwa ya adui yasiwe juu yako ...

Yohana 10:10 ..Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; Mimi (Yesu) nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele

KILA UGONJWA NA UDHAIFU ULIO KWENYE MWILI WAKO SIO WA KWAKO NI WA ADUI, KEMEA KWA JINA LA YESU

OMBA..

YESU ALIKUJA ILI NIWE NA UZIMA TELE, NINAO UZIMA KATIKA JINA LA YESU, YESU ALIJITWIKA UDHAIFU WANGU, KATIKA JINA LA YESU.

MAGONJWA YA MLIPUKO YASINIPATE, KWA MAJINA YAKE. NIKO CHINI YA UVULI WA MWENYENZI MAGONJWA HAYATANIPATA...

Mwaka 2017 sitaangukia katika MAGONJWA ya aina yoyote..

SASA OMBA KWA MANENO YAKO* KAMA UNA udhaifu AU ugonjwa WA AINA Yoyote, OMBA Kemea

Mungu atakujalia utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
We are the Standards! 2017

Tuesday, January 17, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 17

SIKU YA 17 - 17/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KWA NINI HOFU SIYO KIKWAZO KWAKO

Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

UKIONA UNA ROHO YA HOFU UJUE IMETOKA KWA ADUI KWANI MUNGU HAJAKUPA HIYO ROHO KWA HIYO LAZIMA UPINGANE NAYO

MUNGU HUTUPA roho ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi WALA HATUNA roho wa utumwa iletayo hofu; bali tulipokea (kwa Mungu) roho ya kufanywa wana….. WANA WAKO HURU… 

SABABU KWA NINI HUPASWI KUOGOPA

KUNA SABABU NYINGI ZA WATU KUTAKIWA KUOGOPA...

1 Samweli 22:23 Kaa wewe pamoja nami, usiogope; kwa maana yeye atafutaye roho yangu, ndiye atafutaye na roho yako; nawe utakaa kwangu salama.

2 Wafalme 6:16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.

1. BWANA NDIYE AKUFANIKISHAYE…

Zaburi 49:16 Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.

HAUKO PEKE YAKO BWANA YUKO KAZINI NA WEWE…

Isaya 41:10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

1 Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

YESU ALISEMA Mathayo 28:20 …… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. YAANI JANA, LEO NA KUENDELEA

Zaburi 4:8 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

2. MUNGU ANAWEZA KUKUEPUSHA NA AIBU

Isaya 54:4 Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena

3. KUMTUMAINI BWANA HUONDOSHA MBALI HABARI MBAYA…..NA HATA IKIJA HAUTATIKISIKA WALA KUOGOPA

Zaburi 112:7 Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.

Zaburi 23:4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

4. MALAIKA WAKO KAZINI KUHAKIKISHA USALAMA WAKO WALA HATUJILINDI...

Zaburi 34:7 Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Zaburi 91:5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

5. BWANA NDIYE TEGEMEO LETU SIYO WATU…..HATA KAMA WANAWEZA KUTUSAIDIA BWANA ANAWEZA KUMTUMIA MTU/KITU CHOCHOTE

Waebrania 13:6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

Yeremia 17:7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

Mithali 29:25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye Bwana atakuwa salama. 

Zaburi 125:1-2 Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. 

Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa……….MUNGU YUKO PAMOJA NAMI SIKO PEKE YANGU…. Sitaogopa habari mbaya; Moyo wangu u imara namtumaini Bwana……. walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao… Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami.. Sitaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 NATEMBEA NA KUFANYA MAMBO YANGU KWA UJASIRI..…. MWENYE HAKI NI JASIRI KAMA SIMBA

SASA OMBA KWA MANENO YAKO* KAMA UNA TATIZO LA HOFU AU WOGA WA AINA YOYOTE, OMBA

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
We are the Standards! 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 16

SIKU YA 16 - 16/01/2017
Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KATAA UTASA/KUTOKUZAA KWENYE KILA KITU CHAKO

Kutoka 23:26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.

SIYO KUSUDI LA MUNGU KUSHINDWA KUWA PRODUCTIVE/KUZAA KWANI AHADI YAKE KUTOKUWEPO MWENYE KUHARIBU MIMBA, TASA, WALA KUFA KABLA YA KUMALIZA HESABU ZA SIKU ZAKO…

Ayubu 3:7 Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe

SIKU ZA MTU ZINAWEZA KUFANYWA TASA.. UNAWEZA UKAWA UNAPIGA KAZI KWA BIDII LAKINI UKIFANYA EVALUATION NI KAMA ULIKUWA UNALALA TU NYUMBANI..

Ayubu 15:34 Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.

KATI YA MAMBO YANAYOHARIBU NA KUFANYA WATU KUTOKUZAA NI KUTOMCHA MUNGU NA KUTOA RUSHWA/KUPENDELEA… KWANINI RUSHWA NI MBAYA?

Kumbukumbu la Torati 16:19 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. UWEZO WA KUFIKIRI KIMKAKATI KATIKA HAKI UNAPOTEA…

Zaburi 113:9 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha. LAKINI ASHUKURIWE MUNGU AJUAYE KUBADILISHA MAJIRA..ALIYE TASA AWE MAMA MWENYE FURAHA…

Mwanzo 25:21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba

UNAWEZA KUMWOMBA MUNGU AONDOE UTASA KWAKO NA MKEO (MUMEO) NA PIA KWENYE KILA JAMBO UNAOLIFANYA…

NATAMKA UZIMA JUU YA KILA JAMBO NINALOLIFANYA… HAPATAKUWA NA MWENYE KUHARIBU MIMBA, WALA ALIYE TASA, KATIKA NCHI YANGU; NA HESABU YA SIKU ZANGU BWANA ATAITIMIZA. SIISHI KATIKA RUSHWA NA UPENDELEO WALA KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA… KUTOKUZAA, KUTOKUONGEZEKA HAITATAJWA KATIKA MAISHA YAKO KATIKA JINA LA YESU... KWA SABABU Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 UZAO WAKO UONGEZEKE…. KAMA UNATAKA MTOTO UTAPATA MWAKA HUU

SASA OMBA KWA MANENO YAKO

KAMA UNA TATIZO LA KUTOKUZAA KWA MUDA MREFU OMBA HUKU UMEFUNGA NA USOME, 1 Samweli 1:1-28, Mwanzo 11:30, Zaburi 113:9, Luka 1:36-37

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Saturday, January 14, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 14

SIKU YA 14 - 14/01/2017
Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

NAJITENGA NA UFUKARA NAJIUNGAMANISHA NA UTELE

Kuna watu wanajisikia raha kuwa masikini, lakini pia wanaumia wanaposhindwa kuwasaidia watu wenye uhitaji…. Ni hivi wanafanya kama Yakobo 2:15-16

Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?

Lakini Mhubiri anaongezea pia Mhubiri 9:16 Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi

Kumbukumbu la Torati 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

2 Wakorintho 8:9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

NI MPANGO WA MUNGU KUTAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE…. Kwa sababu ina kazi kwa Mungu 2 Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.

ADUI ANAPENDA UOKOKE LAKINI USIWE NA CHOCHOTE, MUNGU AKAMWAMBIA MUSA Kutoka 3:21 Nami nitawapa watu hao kufadhiliwa mbele ya Wamisri; hata itakuwa, hapo mtakapokwenda zenu hamtakwenda kitupu;

LAKINI FARAO AKA REACT MUSA AKASEMA Kutoka 10:9 Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana sikukuu.

BAADA YA PIGO ………… Kutoka 10:24 Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie Bwana; kondoo zenu na ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi.

KIRI NA UOMBE….. USIMPE ADUI AKUZUIE USIINGIE KATIKA UTELE…
Zaburi 23:1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. KUBALI KUONGOZWA NA BWANA KWANI Zaburi 23:2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

MUNGU amenipa nguvu za kupata utajiri; Nimetajirishwa katika vitu vyote ili niwe na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yangu

Kama Yohana alivyoomba 3 Yohana 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. Zaburi 34:9-10

Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema. WATAKUWA NAVYO TELE

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU 

MWAKA 2017 UIMARISHWE KWENYE KIPATO CHAKO….


SASA OMBA KWA MANENO YAKO

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

Friday, January 13, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 13

SIKU YA 13 - 13/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA
KUSHINDA KUAMBATANA NA WATU WASIO SAHIHI/MAHUSIANO MABOVU

Mithali 7:7 Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,

Sikutegemea kijana huyu awe na akili wakati yuko katikati ya wajinga…. Ndiyo maana ni vyema kumwomba Mungu akupe watu sahihi wa kuambatana nao… .SIMAANISHI WALIOKUZIDI TU BALI WANAOTAKIWA (RIGHT PEOPLE) Mithali 13:20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia

Changamoto ya kwanza ya Balaamu haikuwa uchawi wake bali watu waliombatana nao… ndiyo waliomshawishi awalaani Israeli…

MUNGU ANAMUULIZA BALAAMU Hesabu 22:9 Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?

MUNGU AKUFUNDISHE NA AKUSAIDIE KWA ROHO WAKE MTAKATIFU KUCHAGUA WATU SAHIHI MWAKA 2017

Wakati mwingine macho yanaweza kukudanganya ukaingia kichwa kichwa kumbe kuna hila kwa sababu umeangalia kwa nje tu…

KUNA MTU AKIFANYA “FRIENDSHIP ANALYSIS” UTAGUNDUA TANGU UANZE KUKAA NA BAADHI YA WATU UMEENDELEA AU UMERUDI NYUMA…. UNAONGEZEKA AU UNAPUNGUA… KIU YA KUMTAFUTA MUNGU INAZIDI AU INAPUNGUA… ANGALIA TABIA MPYA ULIYOIPATA… NZURI AU MBAYA???

1 Samweli 18:1 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
MUNGU AKUKUTANISHE NA WATU SAHIHI WA KUAMBATANA NAO KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 UWE NA MAHUSIANO SAHIHI KATIKA JINA LA YESU….

SASA OMBA KWA MANENO YAKO

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017